ON STAGE

HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

FORD TANZANIA FACEBOOK

Jumatano, 21 Juni 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI WA RUVU JUU MLANDIZI MKOANI PWANI PIA AZINDUA VIWANDA VINGINE MKOANI HUMO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Archard Mutalemwa  mara baada ya kuzindua mradi huo Mkubwa wa maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia hatua za usafishaji wa maji katika kituo cha kusafisha maji ya Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani, kushoto ni Mtendaji mkuu wa DAWASCO Eng. Cyprian Luhemeja akitoa maelezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa miji ya Pwani na Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ujumbe aliotumiwa na Waziri mkuu wa India Narendra Modi kupitia luninga kabla ya kuzindua Mradi huo wa maji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuzindua Mradi wa maji wa Ruvu juu Mlandizi mkoani Pwani

Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfuko wa sandarusi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilijaribu Trekta mojawapo katika kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kabla ya kufungua kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipeperusha bendera kuashiria kuiruhusu treni ta TRL kusafirisha nondo kutoka kwenye kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   pamoja na viongozi wengine akifungua kiwanda hicho cha nondo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi kwenye sehemu ya kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani. PICHA NA IKULU

Jumatano, 14 Juni 2017

RAIS JP MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA BARRICK GOLD CORPORATION, MMILIKI MKUBWA WA ACACIA MINING LIMITED- ONA VIDEO MUBASHARA

Huyu ndie John Lawson Thornton aliyezaliwa  tarehe 2 Januari 1954. John pamoja na kuwa msomi mzuri ambaye anaendesha Global Leadership Program katika chuo kikuu cha  Tsinghua katika jiji la Beijing China, pia ndie Mwenyekiti Mtendaji wa Barrick Gold Corporation mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mininga Limited, kampuni ambayo iko katikati ya timbwili la usafirishaji tata wa makinikia. Thornton ametua Dar es Salaam na leo amekuwa na mazungumzo na Rais wetu Dr John Pombe Magufuli. Maelezo zaidi soma taarifa hiyo chini kutoka Ikulu Dar es Salaam
video

video


Jumatano, 7 Juni 2017

KIFO CHA CISCO NI MSIBA WA DAR ES SALAAM


Imeandikwa na Benny Kisaka
Abdulkarim Omary Mtiro, almaarufu Cisco  Mtiro, umelala Brother tangulia. 
Umelala usingizi. Usingizi ambao hautaamka wakati huu. Hautaamka brother kwa kuwa wanaolala usingizi huu wanamngoja aliyewaumba awaamshe.
Kwa neema yake kuu iko siku utaamka Brother. Mara hii ukiamka hutalala tena.
Naam, hutalala. Maana utakuwa umevuka ng'ambo ya pili ya mto. Huko hakuna uchungu na maumivu makali kama uliyoyapitia nyakati zako za mwisho za uhai wako ukiwa hospitali ya Aga Khan. Pumzika kaka yetu.
Leo June 7, saa 7 mchana tunakuzika kwenye makaburi ya Kisutu mahali ambapo miezi michache iliyopita tulimzika rafiki yako wa karibu Afande Chicco. Pumzika kwa amani, mpaka tutakapoonana tena huko juu Ng'ambo ya pili.
Mwanadiplomasia uliyewahi kuwa balozi mdogo Nigeria na pia Balozi Kamili nchini Malaysia.
Tunakuita brother kwa wakazi wa Temeke tukijua umezaliwa peke yako kwa Mzee Omary na Bi Ummi Seif. 
Akiwa amezaliwa mtaa Kipata Kariakoo mwaka 1950, baada ya miaka miwili alihamia Temeke hadi anamaliza elimu ya Chuo Kikuu, alihama pale alipoanza kazi wizara ya mambo ya Nje.
Cisco ni jina la utani lililochepua hadi kuliweka rasmi hata kwenye passport yake ikisomeka Abdul Cisco Mtiro amefariki akiwa na miaka 67.
Leo Temeke itanyanyuka eneo ulilokulia na kusoma elimu yako ya msingi shule ya Temeke, na kumaliza elimu hiyo mwaka 1965.
Itakumbukwa 1997 aligombea Ubunge Temeke akishindana na Mrema, viongozi wote wa ngazi za juu wa CCM walikuja kukupigia debe lakini kura hazikutosha.
Umaarufu wako upo Chang'ombe, Ilala, Wailes, Kurasini  Masaki, Magomeni, Mbezi Beach, Kariakoo na hata Kinondoni yote.
Ameishi Mikocheni B hadi umauti umemkuta, lakini muda mwingi amekuwa akikutana na marafiki zake viunga vya Kinondoni kwa John Fedha ama nyuma ya ubalozi wa Ufaransa kijiwe cha Octa.
Ni mmoja wa waanzilishi wa bonanza la kila jpili pale Leaders Club, mshabiki mkubwa wa Yanga, rafiki wa kila tabaka na rika na hakuwa mtu wa kujikweza, umaarufu wake ulitawala kwa kuwa mtu mwenye utani mwingi...
Ni mtoto wa mjini hasa, hakuhitaji aimbwe redioni kutokana na sababu zozote.
Nilikuwepo Kisutu kukuzika bro, ulishiriki msiba wa baba yangu Christopher kisaka, ambaye alikuwa mwalimu wako shuleni Temeke, ulitukaribisha nyumbani kwako kupata chakula cha jioni mara kadhaa tulipofika Kuala Lumpur, Malaysia 2011 nikiwa na Juma Pinto, ulinialika arusi ya mwanao Omary, pia nilishiriki.
Mwanadiplomasia, mkuu wa Itifaki mstaafu kwa Mwalimu Nyerere, Mzee Mkapa na awamu ya nne ya Jakaya Kikwete.
Ulikuwa mgeni rasmi miss Temeke 2003. Ulikuwa judge miss Tanzania 2004.
Cisco ana marafiki lukuki kiasi kila mmoja anaweza kumwandika amjuavyo, tena zaidi na vizuri kutipa mimi, ila kwa udogo huu naomba mwenyezi Mungu akupumzishe kwa Amani🙏

Jumatatu, 5 Juni 2017

KINACHOENDELEA MSIBA WA MAREHEMU CISCO MTIRO


Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro (pichani) ambaye amefariki dunia jana asubuhi  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa siku ya JUMATANO, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo

Mtambo ametoa taarifa kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo yamepangwa kufanyika siku ya JUMATANO saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 
Hiyo ni baada ya kuwasili watoto wake walioko Marekani ambao wanategemewa kuwasili Jumanne usiku, pamoja na mjane wa marehemu anayetegemewa kuwasili Jumanne mchana akitokea Bangui, Afrika ya Kati.
Amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nyumbani kwa marehemu saa tano asubuhi siku hiyo ya JUMATANO ambapo utafanyiwa kisomo na kuswaliwa kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.
 Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.

Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA

Jumapili, 4 Juni 2017

VIONGOZI WAMIMINIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU DKT PHILEMONI NDESAMBURO KUTOA POLE KWA FAMILIA

Maandalizi ya Mazishi ya marehemu Dkt ,Philemoni Ndesamburo yakiendelea nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Kwaya ikihudumu kwa nyimbo kwa ajili ya kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akitoa mkono wa pole kwa mama Mjane wa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo alipotembelea nyumbani kwa marehemu kuifariji familia. 
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ,Freeman Mbowe akitoa mkono wa Pole kwa mjane wa marehemu Dkt Ndesamburo, Ndehorio Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akitoa mkono wa Pole kwa mtoto wa marehemu Dkt Ndesamburo ,Filomena Ndesamburo nyumbani kwao  KDC mjini Moshi.
Waziri wa Malisili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe akitoa pole kwa mama mjane wa marehemu Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa nyumbani kwao.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi, David Mathayo David akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Idd Juma akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo KDC Mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Halmashauri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Mrema akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo KDC mjini Moshi.
Baadhi ya Madiwani wakitia saini katika kitabu cha waombolezaji .
Baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa familia ya marehemu Dkt Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mstaafu ,Saidi Meck Sadiki akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe walipokutana nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo.
Saidi Meck Sadiki akitoa mkono wa pole kwa watoto wa marehemu Dkt Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akisalimiana na mume wa Mbunge wa viti maalumu Lucy Owenya, Dkt Fidelis Owenya alipofika nyumbani wa marehemu Dkt Ndesamburo kutoa salamu za pole.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo Joseph Selasini walipokutana nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Mjane wa marehemu Ndeamburo, Bi Ndehorio Ndesamburo (mwenye nguo za rangi nyeusi ) akionekana ni mwenye huzuni.
Baadhi ya waombolezaji .
Mwenyekiti wa Chadema Taifa  na Kiongozi  wa kambi rasmi Bungeni, Freeman Ndesamburo akisalimiana na Askofu wa KKKT Dkt Martin Shoo alipofika nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo .

Picha na Maelezo na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,
Kanda ya Kaskazini.