HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 25 Machi 2015

DARASA ZIMA WOTE MMEFELI

Hediticha wa shule moja kule Dom katangaza karibu shule nzima imefeli, baada ya darasa hilo kuwa katika shule hiyo kwa miaka mitano. Ticha huyo alitangaza last wiik kwa sauti kubwa, 'Asilimia 80 ya madent hamna kitu kabisaaaa'. Wananchi wanaoishi kando kando na shule walikuwa na haya ya kusema;
Mzee Kauzu-'Ehh ni kweli mimi mwenyewe nilikuwa nawaona wanacheza tu hata darasani wakiingia wanacheza tu ndio nikajisemea kimoyomoyo, hawa watafeli'
Mama Salome-'Ndio wamefeli, tena sio asilimia 80 tu hata huyo hediticha nae kafeli,watafelije asilimia 80 yeye abaki? wote wamefeli'
Denti -'Nani kafeli? Sisi wakali sana, yaani hebu fikiria tuna akili mpaka tunalala darasani, we usituchezee sisi'
Mpaka mtandao huu unaenda hewani ubishi ulikuwa unaendelea

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni