HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 25 Machi 2015

WALA MIMI SIKUWAITA NASHANGAA

Yaani we acha tu. Mi nilikuwa niko sebuleni kwangu nimetulia, nakunywa chai yangu taratibu, sina neno na mtu, ghafla si nikasikia nje kuna kelele watu wamejaa mbele ya nyumba yangu. Nikashangaa sana, unajua mi ni mtu mpole sipendagi kelele, nikatoka nje nikashangaa kukuta eti watu kibao wamebeba mabango wanapiga kelele, "Wewe tu mzee wewe tu". Unajua siku hizi kuna mikasa mingi, nikajua sijui labda wananifananisha na jambazi. Mwili ukawa unatetemeka, nikawa nafikiria kukimbia. Ndio akajitokeza mzee mmoja wala simfahamu, akanambia, "Mkuu sisi wote tumeoteshwa kuwa unafaa kuwa mwenyekiti wetu wa serikali ya mtaa, hivyo tukajikuta tuu tumefika hapa kwako" Nilishangaa sana kwa upendo mkubwa wa hawa wanamtaa wenzangu, basi si unajua mi mpole ndio nikaona niwakubali kishingo upande. Nikasema," Kwa kweli mi sitaki hicho cheo lakini kwa kuwa mnanilazimisha, basi nikikipata ntawaletea kila nyumba chai maandazi kila siku, halafu ntahakikisha hakuna mtu anafanya tena dhambi mtaa huu. Wote tutaanza kuishi kama peponi' Ndio kishingo upande nikajisemea kimoyomoyo, "Ok ngoja niwe Mwenyekiti" Kuangalia kushoto kwa nyumba yangu nikapata shock, kumbe watoto wangu walikuwa wamekwisha wapangia viti wale wageni waliokuja ghafla, wakawa wamewawekea na matenti na chai na makeki, yaani mwenyewe nikashangaa. Basi ndio nikakaa na wananchi wenzangu nikala nao chakula cha mchana nikawapa nauli wakaondoka kurudi kwao kwa furaha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni