HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 21 Aprili 2015

KUCHINJA NA KULA NYAMA YA NG'OMBE MARUFUKU-SOMA KIOJA HICHO


Ni kama wiki sita zimepita toka jimbo moja kubwa huko India, jimbo la  Maharashtra, limepiga marufuku uuzaji na utumiaji wa nyama ya ng’ombe. Kumekuweko na malalamiko kutoka kwa wananchi wa jimbo hilo ambalo maisha yao yanategemea nyama ya ng’ombe, lakini mji mmoja ulioko katika jimbo hilo umeboresha zaidi staili yake kuhakikisha sheria hiyo inafuatwa kikamilifu. Polisi wa mji wa Malegaon Magharibi mwa India, ili kuhakikisha hakuna ng’ombe anaechinjwa, wamekuwa wakipiga picha kila ng’ombe akiwa amesimama na mwenye mfugo huo. Na jedwali limeandaliwa ambalo picha hizi ziko katika hifadhi ya polisi sasa ole wako ng’ombe uliyepiga nae picha asionekane. 
Uchinjaji wa ng’ombe ulipigwa marufuku katika jimbo hilo kuanzia mwaka 1976, sheria hiyo imeleta kelele kuwa serikali ya jimbo hilo ambalo linaongozwa na chama cha Bharatiya Janata Party  chenye Wahindu wengi, inawanyanyasa watu wa dini nyingine ambao kwao ng’ombe ni mfugo tuu. WaHindu huona ng’ombe ni kitu kitakatifu, na huachiwa kufanya chochote ambacho ng'ombe anataka.
Kama kawaida katika kila timbwili kuna wanaofaidika, kati ya kundi lililofurahi katika kuja kwa sheria hii ni wapiga picha wa jimbo hilo ambao wanasema wanatengeza pesa nyingi kwani kila ng’ombe picha moja.

Ijumaa, 10 Aprili 2015

ALIYEACHISHWA KAZI NA WAZIRI KUMBE ALIKWAJIACHISHA KAZI LONG TAIM EGOOO


JANA KATANGAZWA KASITISHWA KAZI NA WAZIRI, LEO KASEMA ALIKWISHA ACHA KAZI SIKU NYIIIIIIIIIINGI. HII POLITIKI TAMU SANA, YAAAANI WASHAURI WALIMUINGIZA MKENGE  MKUU KUWA JAMAA BADO YUKO OFISINI? AU MKUU ALICHUKUA HATUA BILA USHAURI WA VIJANA WAKE? NA JE ALIYESTAAFUU ALISHIRIKI KWENYE  ISHU? NA WHAT NEXT??? SUBIRI HAPA HAPA CHEKA POLITIKI USITOKE WE NGOJA SERIKALI YETU SIKIVU ITA TEK STRONG EKSHEN

Jumatano, 8 Aprili 2015

BINGWA WA WIZI WA KURA UNAMJUA?

ALIWAHI kuwa Rais wa Liberia ambaye sasa yumo kwenye kitabu cha Guiness, kwa kuwa bingwa wa wizi wa kura. Bingwa huyu pichani, alishinda uchaguzi mwaka 1927 nchini mwake kwa wingi wa kura 234,000. Japokuwa wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 15,000 tu. Haya tunataka Bongo nayo ing'are kwenye kitabu cha Guiness, jitahidini wahusika

Jumatano, 1 Aprili 2015

MAPICHA YA VICHEKESHO YA POLITIKI ZA UCHAGUZI NAIJERIAPOLITIKI NAIJERIA, ALIWAHI KUTAWALA KIJESHI, SASA KAINGIA KWA KURA


Gen Muhammadu Buhari, ambaye aliwahi kuongoza Naijeria kijeshi kuanzia tarehe 31 Desemba 1983 mpaka 27 Agosti 1985, baada ya kupindua serikali, hatimae amerudi tena madarakani kwa njia ya kura hahahahaha.
 Ni mara ya kwanza kwa politiki za Naijeria upinzani ukashinda uchaguzi kwa kupitia kura. Wachunguzi wanasema mambo matatu ambayo yaliiondoa serikali iliyokuwa madarakani ni;
1.   Rushwa
2.   Ukosefu wa ajira
3.   Usalama wa wananchi , hasa kuhusu tishio la Boko Haram
Haya wanapolitiki wa TZ mnajifunza nini? Msianze kushangilia tu ohooo