HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 21 Aprili 2015

KUCHINJA NA KULA NYAMA YA NG'OMBE MARUFUKU-SOMA KIOJA HICHO


Ni kama wiki sita zimepita toka jimbo moja kubwa huko India, jimbo la  Maharashtra, limepiga marufuku uuzaji na utumiaji wa nyama ya ng’ombe. Kumekuweko na malalamiko kutoka kwa wananchi wa jimbo hilo ambalo maisha yao yanategemea nyama ya ng’ombe, lakini mji mmoja ulioko katika jimbo hilo umeboresha zaidi staili yake kuhakikisha sheria hiyo inafuatwa kikamilifu. Polisi wa mji wa Malegaon Magharibi mwa India, ili kuhakikisha hakuna ng’ombe anaechinjwa, wamekuwa wakipiga picha kila ng’ombe akiwa amesimama na mwenye mfugo huo. Na jedwali limeandaliwa ambalo picha hizi ziko katika hifadhi ya polisi sasa ole wako ng’ombe uliyepiga nae picha asionekane. 
Uchinjaji wa ng’ombe ulipigwa marufuku katika jimbo hilo kuanzia mwaka 1976, sheria hiyo imeleta kelele kuwa serikali ya jimbo hilo ambalo linaongozwa na chama cha Bharatiya Janata Party  chenye Wahindu wengi, inawanyanyasa watu wa dini nyingine ambao kwao ng’ombe ni mfugo tuu. WaHindu huona ng’ombe ni kitu kitakatifu, na huachiwa kufanya chochote ambacho ng'ombe anataka.
Kama kawaida katika kila timbwili kuna wanaofaidika, kati ya kundi lililofurahi katika kuja kwa sheria hii ni wapiga picha wa jimbo hilo ambao wanasema wanatengeza pesa nyingi kwani kila ng’ombe picha moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni