HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 15 Mei 2015

POLITIKI BURUNDI EPISODE 2


Rais Pierre Nkurunziza amesema kuwa yeye kisharudi Burundi, ishu imepostiwa kwenye akaunti Twitter ya Rais huyo. Katika twit hiyo taarifa hiyo imetolewa na pia taarifa imesema kuwa jaribio la mapinduzi limeshindwa na Rais ataongea na wananchi wake leo Ijumaa. 
Mpaka jana jioni inasemekana kulikuwa na mapigano ya kugombea jengo la radio ya Taifa, jambo linaloonyesha bado kuna wanaopinga Nkurunziza kurudi madarakani.Bado kulikuwa hakuna taarifa ya aliko Rais Nkurunziza, japokuwa mashirika mengi ya habari na hata Twit hii inaonyesha mkuu huyo yuko ndani ya nyumba Burundi. General Cyrille Ndayirukiye, aliyekuwa msaidizi wa kiongozi wa mapinduzi alikiri kuwa jaribio lao limeshindwa. Alisema  "Tulikutana na upinzani mkali uliokuwa unaunga mkono watu walioko madarakani."  Mkuu wa majeshi, Chief of Staff General Prime Niyongabo pia alisema jaribio hilo limeshindwa. Katika tangazo lililotolewa mapema Nkurunziza alisema “Nawashukuru sana askari waliohakikisha kila kitu kiko salama na nina wasamehe wote waliojaribu kunipindua”
Umoja wa Mataifa umelaani pande zote husika, umelaani wale wanaotaka kufanya mapinduzi na wale wanaotaka kuchukua madaraka kwa kutumia njia zisizo halali. Umoja wa Mataifa pia umegawanyika katika swala la Burundi, Urusi na China wakiwa na msimamo kuwa swala la muhula wa tatu ni swala la Kikatiba la nchi ya Burundi hivyo nchi iachiwe iamue yenyewe.

Alhamisi, 14 Mei 2015

POLITIKI ZA BUJUMBURA, NKURUNZIZA YU WAPI?


Kizungumkuti cha Politiki za Burundi kinaendelea. Kumekucha na asubuhi nyingine na wakazi wa Bujumbura wanaonekana hawaelewi nini kinaendelea. Nani yuko madarakani baada ya taarifa za jana kuwa serikali ya nchi hiyo imeondolewa madarakani? Mara baada ya tangazo hilo jana wananchi kwa mamia walitoka nje wakiimba na kusherehekea kile kilichoonekan ni ushindi kwao wa kupinga Rais Nkurunziza kujaribu kuongeza awamu nyingine madarakani. Lakini muda mchache baadae wakapata taarifa kinyume kuwa jaribio lilikuwepo lakini limeshindwa. Inaonekana kuna mgawanyiko jeshini kati ya wanaompinga na wanaomuunga mkono Nkurunziza, na inasemekana kuwa pande hizo mbili zimo katika mazungumzo ya kuangalia namna ya kwenda mbele.
Jaribio hili la mapinduzi lilifanyika wakati Nkurunziza akiwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano uliohusu kilichokuwa kikiendelea katika nchi yake. Upande uliokuwa ukimuunga mkono  Nkurunziza, ulitoa taarifa  kupitia ukurasa wa Twitter na Facebook wa Rais Nkurunziza, kuwa kulikuweko na jaribio la kumpindua Rais lakini limeshindwa. Haijulikani Rais huyo yuko wapi kwa muda huu kwani ndege yake ilizuiwa kutua Burundi na ikatua katika uwanja wa ndege wa Entebbe, baada ya hapo haijulikani kama bado yuko Uganda au yuko Tanzania kama vyombo vingi vya habari vinavyosema.

Jumatatu, 4 Mei 2015

KIMENUKA POLITIKI ZA ARUSHA,


Zaidi ya vijana 1000 wamfanya maandamo katika jiji la Arusha wakimpinga Mbunge wao machachari Mh. Godbless Leman a wakitaka asigombee tena jimbo hilo. Kisa kikubwa kikiwa kuwa Mbunge huo ndie amekuwa chanzo cha hali ngumu katika jiji hili kinara la utalii. Mayanki hao wanadai Mbunge huo ameleta balaa na cham chao kisipomteua mgombea tofauti mwaka huu basi kura zao zitaenda CCM.
Rashid Mbakizao ambaye anadai kuwa likuwa Katibu wa Mkoa wa Arusha kwa miaka mingi anasema simu yake ilikuwa na namba karibu 3000 za vijana ambazo kila akitumwa kuleta sokomoko alikuwa akiwapigia kuwataarifu kabla ya maandamano. Sasa lalamikao nikuwa walioumia walioharibikiwa kibiashara waliahidiwa kulipwa lakini imekuwa kimyaaaaa.
Viongozi wa CHADEMA wanasema vijana hao wamenunuliwa na maadui wa cham chao.

Jumamosi, 2 Mei 2015

UNAJUA MEI DEI ILIANZANJE?

Leo Mei Mosi,wafanyakazi wamesherehekea siku ya Wafanyakazi, Mei Dei lakini unajua ilianzaje? Turudi nyuma mpaka tarehe 1 May 1886, Wafanya kazi 200,000 wa Marekani wakagoma wakidai kuwa wawe wanafanya kazi kwa masaa manane tu kwa siku. Siku hiyo, katika jiji la Chicago na miji mingine jirani wafanya kazi waligoma wakidai haki hiyo. Siku ya May 3 katika kiwanda kilichoitwa McCormick Reaper, mgomo ukageuka mapambano, na kesho yake mkutano wa amani ulioitwa baina ya waajiri na wafanyakazi ukabadilika kuwa mpambano mkubwa. Wanahistoria wanahadithia kuwa siku ya tarehe 4 May 1886 kiasi kama saa nne usiku mvua kubwa ilianza katika jiji la Chicago, waandamanaji waliokuwa wamekusanyika Haymarket Square, walianza taratibu kusambaratika, kabala ya hapo inasemekana walikuweko kama waandamanaji 3000 wakisikiliza hotuba za kulaani ukatiri wa polisi katika kudhibiti maandamano hayo, na huku madai ya siku ya kazi kuwa masaa manane yakiendelea, hivyo mvua ikawakimbiza wengi, hata Meya wa jiji aliyekuwa akitegemea fujo akawa kajua kuwa mambo yameisha na kuelekea kwake kulala. Msemaji wa mwisho alikuwa akimalizia mazungumzo yake ghafla polisi kama 180 wakaingia katika uwanja ule. Mkuu wa polisi akaamrisha watu watawanyike, ghafla bomu likatupwa kwenye kundi la polisi na kujeruhi polisi 67 na kuuwa saba. Hapohapo polisi wakaanza kutumia risasi za moto na kuuwa waandamanaji kadhaa na 200 wakajeruhiwa. Yaliyotokea Haymarket Square yakawa sehemu ya historia ya Marekani. Mwaka 1889 katika mkutano wa International Socialist Conference, ndipo ikatamkwa kuwa kwa kuweka kumbukumbu ya yaliyotokea Haymarket, May 1 iwe ni siku ya kimataifa ya mapumziko ya wafanyakazi. Kutokana na siasa za Marekani kupingana na usoshalist, mwaka 1958 Rais Eisenhower wa Marekani akatangaza kuwa May moja iwe Loyalty Day, siku ya kuonyesha uaminifu kwa nchi ya Marekani na kutambua Uhuru wa Wamarekani. Pamoja na kwamba siku hiyo ilianza Marekani , nchi hiyo husherehekea siku ya wafanyakazi mwezi September.