HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 15 Mei 2015

POLITIKI BURUNDI EPISODE 2


Rais Pierre Nkurunziza amesema kuwa yeye kisharudi Burundi, ishu imepostiwa kwenye akaunti Twitter ya Rais huyo. Katika twit hiyo taarifa hiyo imetolewa na pia taarifa imesema kuwa jaribio la mapinduzi limeshindwa na Rais ataongea na wananchi wake leo Ijumaa. 
Mpaka jana jioni inasemekana kulikuwa na mapigano ya kugombea jengo la radio ya Taifa, jambo linaloonyesha bado kuna wanaopinga Nkurunziza kurudi madarakani.Bado kulikuwa hakuna taarifa ya aliko Rais Nkurunziza, japokuwa mashirika mengi ya habari na hata Twit hii inaonyesha mkuu huyo yuko ndani ya nyumba Burundi. General Cyrille Ndayirukiye, aliyekuwa msaidizi wa kiongozi wa mapinduzi alikiri kuwa jaribio lao limeshindwa. Alisema  "Tulikutana na upinzani mkali uliokuwa unaunga mkono watu walioko madarakani."  Mkuu wa majeshi, Chief of Staff General Prime Niyongabo pia alisema jaribio hilo limeshindwa. Katika tangazo lililotolewa mapema Nkurunziza alisema “Nawashukuru sana askari waliohakikisha kila kitu kiko salama na nina wasamehe wote waliojaribu kunipindua”
Umoja wa Mataifa umelaani pande zote husika, umelaani wale wanaotaka kufanya mapinduzi na wale wanaotaka kuchukua madaraka kwa kutumia njia zisizo halali. Umoja wa Mataifa pia umegawanyika katika swala la Burundi, Urusi na China wakiwa na msimamo kuwa swala la muhula wa tatu ni swala la Kikatiba la nchi ya Burundi hivyo nchi iachiwe iamue yenyewe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni