HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Alhamisi, 14 Mei 2015

POLITIKI ZA BUJUMBURA, NKURUNZIZA YU WAPI?


Kizungumkuti cha Politiki za Burundi kinaendelea. Kumekucha na asubuhi nyingine na wakazi wa Bujumbura wanaonekana hawaelewi nini kinaendelea. Nani yuko madarakani baada ya taarifa za jana kuwa serikali ya nchi hiyo imeondolewa madarakani? Mara baada ya tangazo hilo jana wananchi kwa mamia walitoka nje wakiimba na kusherehekea kile kilichoonekan ni ushindi kwao wa kupinga Rais Nkurunziza kujaribu kuongeza awamu nyingine madarakani. Lakini muda mchache baadae wakapata taarifa kinyume kuwa jaribio lilikuwepo lakini limeshindwa. Inaonekana kuna mgawanyiko jeshini kati ya wanaompinga na wanaomuunga mkono Nkurunziza, na inasemekana kuwa pande hizo mbili zimo katika mazungumzo ya kuangalia namna ya kwenda mbele.
Jaribio hili la mapinduzi lilifanyika wakati Nkurunziza akiwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano uliohusu kilichokuwa kikiendelea katika nchi yake. Upande uliokuwa ukimuunga mkono  Nkurunziza, ulitoa taarifa  kupitia ukurasa wa Twitter na Facebook wa Rais Nkurunziza, kuwa kulikuweko na jaribio la kumpindua Rais lakini limeshindwa. Haijulikani Rais huyo yuko wapi kwa muda huu kwani ndege yake ilizuiwa kutua Burundi na ikatua katika uwanja wa ndege wa Entebbe, baada ya hapo haijulikani kama bado yuko Uganda au yuko Tanzania kama vyombo vingi vya habari vinavyosema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni