HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatatu, 24 Agosti 2015

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI 2015


Chama Cha Mapinduzi CCM, jana tarehe 23 August 2015, kilizindua kwa kishindo kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam. Maelfu ya watu walihudhuria mkutano huo ambao kwa kila hali ulifana sana. Uzinduzi huu ulishereheshwa na wasanii mbalimbali kama ambavyo imekuwa kwa kampeni za chaguzi zilizopita, miaka ya nyuma bendi maarufu zilizokuweko wakati huo ndizo zilishirikiana na TOT kunogesha shughuli, mwaka huu wasanii wa kizazi kipya walifanya shughuli hiyo..Viongozi wa nchi wastaafu wenye heshima kubwa katika jamii walikuweko na kutoa wosia wao kwa waTanzania kuhusu uchaguzi ujao ambapo wote walitoa sifa za mgombea John Pombe Magufuli na mgombea mwenza mama Samia Suluhu.

Safari ndio hiyo imeanza  fuatilia blog hii kwa habari vituko hadithi za safari hii ya ushindi kila siku

Wagombea wakinyanyua Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015Wasanii mbalimbali wakifurahia uzinduzi wa kampeni
Nnape Nnauye mbele ya umati mkubwa uliohudhuria uzinduzi huo
Katika hotuba yake mgombea John Pombe Magufuli ametaja mambo mengi ambayo ameahidi kuyashughulikia kati ya hayo ni
·      Umoja wa Taifa
·      Kulinda Muungano wa Tanzania
·      Kuhakikisha Ulinzi na Usalama wan chi
·      Utawala bora
·      Mahakama maalumu kwa mafisadi na majizi
·      Kuongeza ajira kwa kuimarisha viwanda, kilimo na mifugo
·      Kuhakikisha wanaotakiwa kulipa kodi wanalipa kodi
·      Gesi kutumiwa vyema,
·      Kuimarisha miundo mbinu
·      Kuboresha hali ya wasanii na wanamichezo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni