CHEKA LAKINI USILIE


Miaka michache iliyopita mwanasiasa mmoja masikini wa Bongo alikwenda Brazil kikazi, kule akakutana na mwanasiasa mmoja wa kule tajiri sana. Ikalazimika amuulize,
MBONGO: Najua wewe ni kiongozi wa serikali unakuwaje tajiri hivyo?
MBRAZIL: Hebu chungulia hapo nje unaona barabara hiyo?
MBONGO: Ndio naiona nzuri sana
MBRAZILI: Basi hapo nimepata 10%.
Miaka michache baadae Mwanasiasa Mbrazil alitembelea Bongo akamkuta yule mwanasiasa Mbongo kawa ni tajiri wa kutupwa.
MBRAZIL: Mwenzangu, umewezaje ghafla kuwa tajiri hivyo?
MBONGO: Hebu chungulia hapo nje, unaliona daraja hilo?
MBRAZIL: Sioni daraja lolote?
MBONGO: Basi hapo nimepata 100%


Maoni