HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 29 Septemba 2015

MAMA SAMIA SULUHU, MGOMBEA MWENZA ALIYEPANGA KUWAPIGANIA WANAWAKE

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.
 MCHUANO wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika Oktoba 25, 2015 unaendelea maeneo mbalimbali ya nchini, huku vyama anuai vilivyofanikiwa kuingia katika ushindani huo wa kisiasa vikinadi ilani na sera zao kwa Watanzania ili kuwashawishi wachaguliwe. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara ya kwanza kimemsimamisha mwanamke katika ngazi ya juu ya uongozi. Kimemteuwa mwanamama, Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, John Pombe Magufuli. Kwa mantiki hiyo endapo kitafanikiwa kushinda urais Tanzania kwa mara ya kwanza mwanamke atashika nafasi ya juu ya madaraka ndani ya Serikali. Bi. Suluhu ambaye amewahi kufanya kazi kama kiongozi katika Serikali zote mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar-SMZ) anauzoevu wa kutosha na elimu nzuri inayomuongeze sifa ya kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa. Ki historia, Bi. Suluhu alizaliwa Januari 27, mwaka 1960 nchini na kupata elimu yake ya msingi na sekondari Zanzibar, kabla ya kuendelea na elimu ya juu kwa kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya Mzumbe nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Huri cha Tanzania (OUT). Mwanamama huyu pia amefanikiwa kuchukua kozi ndogo ndogo anuai katika vyuo vya ndani na nje ya Tanzania, vikiwemo vya; 'Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India', Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA, pamoja na National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan. Mgombea huyo mwanamama amekuwa waziri na mbunge kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo na pia kufanikiwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, nafasi ambazo kwa kiasi kikubwa zinamuongezea sifa ya kuweza kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa anasema hii ni nafasi pekee kwa akinamama wote bila kujali itikadi zao kumuunga mkono ili aweze kushinda na kuweka historia nchini ya mwanamke kushika nafasi ya juu kuliko zote nchini. Kwa sasa kiongozi huyu anazunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani kuinadi ilani ya CCM. Bi. Suluhu anasema ilani ya CCM imepanga kufanya mengi mazuri kwa Watanzania, lakini pamoja na hayo amejitolea kuhakikisha anawapigania akinamama endapo atafanikiwa kushinda nafasi hiyo ili kuweza kukabiliana na changamoto anuai ambazo zimekuwa kero na kikwazo kwao. Anazitaja changamoto hizo ni pamoja na huduma za afya ya uzazi ambapo akinamama wengi na watoto wachanga wamekuwa wakipoteza maisha katika eneo hilo. Anasema licha ya ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kufafanua zaidi itakavyo boresha huduma za afya kiujumla, lakini atalisimamia na kuongeza nguvu za ziada kuhakikisha akinamama wanapata huduma za kuridhisha maeneo wanapopata huduma za afya ya uzazi. Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Mbulu Mjini anasema endapo CCM itashinda uchaguzi huu imepanga kuajiri watumishi 15,000 wa sekta ya afya wakiwemo madaktari 2020 ndani ya kipindi kifupi ili kuhakikisha inaboresha zaidi huduma za afya maeneo mbalimbali nchini hasa huduma za akinamama na watoto. Bi. Suluhu anasema hatua hiyo ni mpango maalumu wa kuboresha huduma za afya kiujumla na hasa huduma za akinamama wajawazito na watoto ambapo wamekuwa na changamoto katika huduma hizo.  Aidha anaongeza kuwa mpango mwingine ni kuwawezesha akinamama na vijana kiuchumi kupitia vikundi vyao. Anabainisha kuwa eneo hili Serikali ya CCM kupitia ilani yake imetenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji fedha ambazo zitakuwa zikikopeshwa makundi hayo kwa masharti nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi. Anasema eneo hilo pia halmashauri zitasimamiwa kutoa asilimia tano ya mapato kuwaunga mkono akinamama na vijana ili kuchochea maendeleo yao. Ili kukuza biashara zao Bi. Suluhu anasema Serikali itasimamia kuhakikisha asilimia 30 ya tenda ndogondogo za halmashauri mbalimbali zipewe vikundi vya akinamama na vijana. Anaeleza kuwa ili kuongeza thamani kwa mazao yatakaokuwa yakizalishwa na vikundi hivyo kupitia miradi ya kilimo imepanga kujenga viwanda vingi maeneo mbalimbali ya nchi ambavyo vitayaongezea thamani mazao na pia kuzalisha ajira kwa asilimia 40, jambo ambalo pia litakuza uchumi wa akinamama na vijana. Mwanamama huyo shupavu anabainisha kuwa kutokana na suala la kero ya maji pia kuwaumiza zaidi akinamama ilani ya chama chake imedhamiria kumalizia miradi ya maji na kuanzisha mingine anuai ili kukabiliana na changamoto ya kero ya maji safi na salama iliyopo maeneo mbalimbali ya nchini vijijini ama mjini. Bi. Suluhu anasema Serikali watakayoiunda itaendelea kushughulikia kero ya maji katika vijiji vyenye ukame na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama kwa matumizi. Lakini ili kumaliza kabisa kero hiyo anasema Serikali itaunda mfuko wa maji ambao utashughulikia kero za huduma za maji safi na salama. Anasema migogoro yoyote inayosababisha mapigano idadi kuwa inayoathirika ni wanawake na watoto, hivyo Serikali itakayoundwa na CCM itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na Wilaya na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi inayochangia mapigano ya wakulima na wafugaji baadhi ya maeneo ya Tanzania mara kwa mara.  Anasema mara baada ya kupima ardhi na kuweka mipaka kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji watahakikisha mipaka hiyo inatambulika na kuheshimiwa na jamii zote mbili ili kuzuia migogoro na mapigano ambayo yamekuwa na uhasama mkubwa na kupoteza uhai na mali za raia wasio kuwa na hatia katika maeneo yenye mgogoro. Hata hivyo katika kampeni zake mara zote amemalizia kwa kuwaomba wananchi kutunza amani iliyoasisiwa na viongozi wetu wa taifa kwa kutokubali kuyumbishwa na kushawishia kuvuruga amani ya nchi. "...Tusikubali kuchokozwa na kuchokoseka na kuvuruga amani...bila amani hakuna maendeleo," alisema Bi. Suluhu. Anawataka viongozi wa siasa kuacha kutoa vitisho kwa wapiga kura kwani hali hiyo ni kuibaka demokrasia hivyo CCM na vijana wake hawatakuwa tayari kuona demokrasia inabakwa nchini na wapuuzi wachahe. "Miongoni mwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kulingana na taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni pamoja na CCM, CUF, CHADEMA, UMD, NCCR- Mageuzi, NLD, UPDP, NRA, TADEA, TLP, UDP, DEMOKRASIA MAKINI, CHAUSTA, DP, APPT-Maendeleo, Jahazi Asilia, SAU, AFP, CCK, ADC, CHAUMMA na ACT-Wazalendo. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

BADO NAJIULIZA MGOMBEA ALIKUWA ANAENDA WAPI?- VIDEO


WASANII WA BONGO MOVIE WAIBUKIA MJINI IRINGA,WATANGAZA KUTEMBEA NCHI NZIMA KWA BAJAJ KUMUUNGA MKONO DKT MAGUFULI


Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-IRINGA
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda  nafasi ya Urais.
  Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika) ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
 Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,jioni ya leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Magufulika staili kama kawa, hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo jioni ya leo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini, la kupiga push up kama ionekanavyo pichani.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani Iringa.
  Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda
Ngoma ya livangala ikitumia vinu ilikuwa kati ya vi mbwanga vya hapa na pale vilikuwepo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ifunda mapema leo mchana
Wazee wa kimila wa kabila la Wahehe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema leo mchana katika Mji wa Ilula Jimbo la Kilolo mkoani Iringa.
  Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.
 Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Samora wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
 Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakifuatilia mkutano wa kampeni,wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano

Jumatatu, 28 Septemba 2015

MUONE MAMA OBAMA AKI MAGUFULIKA WE UNANGOJA NINI?- VIDEO


MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE NDANI YA CHIMALA,MBARALI,MAKAMBAKO NA MAFINGA,


 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaiambisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Mafinga mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
 Mmoja wa Waangalizi wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Makambako jioni ya leo Septemba 27 mkoani Iringa
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  ambaye anashuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vyaWambi  mjini Mafinga mkoani Iringa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.

Dk. John Pombe Magufuli amewaambia wakazi hao wasihadaike na maneno ya kisiasa yanayotolewa na vyama vingine kuwa nchi ya Tanzania haijapiga hatua ikiwa chini ya utawala wa CCM wakati maendeleo yanaonekana wazi na nchi inazidi kusonga mbele kwa mambo mengi ikiwemo amani na utulivu wa nchi.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa  Chimala,Mbarali mkoani Mbeya alipokuwa akielekea mkoani Iringa kuendelea na kampeni zake.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akionesha hisia zake mara baada ya kuonana uso kwa uso na Kada Mkongwe wa chama cha CCM Ndugu Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kada Mkongwe wa chama cha CCM Ndugu Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni,huku Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Ndugu  Bulembo akifuatilia kwa makini
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini katika viwanja vya Barafu mjini Rujewa,wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga a.k.a Jah People akimuombea kura  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini Ilembula leo Septemba 27 mkoni Mbeya
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Injinia Gerson Rwenge,katika mji wa Ilembula
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mjini Makambako kwenye uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 wakazi wa Makambako wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipanda jukwaani kwa kuruka ruka kuonesha yuko fiti kuwatumikia wananchi kwa namna yoyote ile.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah Bulembo akiwahutubia wakazi wa Makambako kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli leo Septemba 27 mkoani Iringa
 Dkt Magufuli akiwasalimia wananchi wa Makambako kabla ya kuanza kuwahutubia na kuwaomba kura
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makambako gombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaimbisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wananchi wa mji wa Makambako wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuwaomba wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 27 kwa kumpiga kura ya ndio na hatimae aibuke mshindi kwa nafasi ya Urais
Picha na Hadithi na Michuzi Jnr