HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 15 Septemba 2015

MSAFARA WA RAIS LUNGU WA ZAMBIA WAPIGWA MAWE


Polisi wa Solwezi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu ili Rais Edgar Lungu aweze kupita wakati akitokea uwanja wa ndege. Wakazi hao wa sehemu ya Kyawama walitupia mawe msafara wa wa Rais Lungu wakimlaumu kwa kudidimiza uchumi. Edgar Lungu amekuwa Rais wa zambia kuanzia January mwaka huu baada ya kifo cha Rais wa awali Michael Sata. Katika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Rais aliyefariki uliofanyika January mwaka huu alimshinda mpinzani wake Hakainde Hichilema kwa kura chache.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni