HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Alhamisi, 15 Oktoba 2015

DR MAGUFULI AHUTUBIA PEMBA LEO


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.

Katika mkutano huo wa Kampeni,Dkt Magufuli ameahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano,atadumisha na kuulinda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ulioanzishwa na Waasisi wetu akiwemo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere pamoja na Abeid Amani Karume. Dkt Magufuli kesho atahutubia kwenye mkutano mkubwa wa kampeni mjini Unguja.
Wananchi wa Kisiwani Pemba wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale ,wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kura kwa wananchi hao. 
Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.Dkt Shein amewataka wakazi wa Kisiwani Pemba kuilinda amani iliyopo ndani ya kisiwa hicho na kuwa Wananchi wakajitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu Mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana Mama Shadia Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Gombani ya Kale kwa ajili ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein kabla ya mkutano wa kampeni kuanza jioni ya leo kisiwani Pemba.
Umati wa wakazi wa kisiwani Pemba kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa kisiwani Pemba wakifuatilia mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo,kwenye uwanja wa Gombani ya kale kisiwani humo.
Wananchi wa kisiwani Pemba wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein walitumia jukwaa na mkutano huo kuwaomba kura za kutosha ili wakaiongoze Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.

PICHA NA MICHUZI JR-PEMBA


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni