HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 2 Oktoba 2015

WASANII WALISHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA SIASA TOKA ENZI ZA KUPIGANIA UHURU WA NCHI HII

TOKEA ENZI za kupigania Uhuru, wasanii walikuwa bega kwa bega wakihamasisha wananchi kujua haki zao na hivyo kudai haki yao ya kupata Uhuru. Kazi za wasanii nyingine zilifika mpaka kupigwa marufuku na hata wasanii wengine walifungwa kwani walionekana kuwa wanachochea ari ya kutaka kumuondoa mkoloni. Wimbo ya Cuban Marimba, Kuku watatu ulionekana wazi unahamasisha ushindi wa Mwafrika katika kupigania Uhuru. Wimbo wa Frank Humplink I am a democrat ulitumia kila kabla ya mikutano ya Mwalimu Nyerere  ya kudai Uhuru. Anaejua historia hakika anafahamu kuwa Mzee Rashid Mfaume Kawawa kwanza alikuwa muigizaji mzuri wa filamu na ndie mwenye  jina la Muhogo Mchungu. Bibi Titi Mohamed alikuwa muimbaji wa kundi la Taarab huko Temeke, Mzee Moses Nnauye alikuwa msanii marufu kusini akihamasisha watu kupitia vikundi vya Tanu Youth League. Ushahidi umejaa kwenye maktaba zetu za Radio Tanzania kazi kubwa ambayo ilifanywa a wasanii hata baada ya Uhuru kuhamasisha kila nyanja ya maisha, kilimo, afya, siasa, amani, ukombozi wa Afrika, na kazi kubwa iliyofanywa na wasanii wakati wa vita na Idd Amin. Hivyo anaebeza au kukasirika wasanii kushiriki katika kampeni za kisiasa hajui historia yake. Kuna kila sababu ya Taifa hili kuangalia upya nafasi ya msani na haki zake za msingi katika awamu ijayo ya uongozi. Kutengeneza mifumo stahiki itakayojali kulinda na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania na kulinda na kuendeleza tasnia nzima ya biashara zitokanazo na kazi za sanaa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni