HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 27 Novemba 2015

NHIF YAKABIDHIWA KITUO CHA MATIBABUCHA MFANO DODOMA


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika. Makadhiano hayo yamefanyika mjini Dodoma leo Ijumaa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa wa Dodoma na timu ya wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo kampuni ya Nosuto Associates. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando, amesema kukamilika kwa jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili kuanza kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi. Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF. Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji wa madai na utambuzi wa wagonjwa. Kaimu Mkurugenzi mkuu pia alisema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa. Naye Mkurugenzi wa fedha, mipango na uwekezaji wa NHIF Bw Desudedit Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania. Picha za kituoSehemu ya  mapokezi  ya kituo cha matibabu cha mfano cha NHIF Dodoma Sehemu ya mapokezi ya kituo cha matibabu cha mfano cha NHIF Dodoma
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando akionesha funguo za Jengo la Kituo cha Mfano cha NHIF Dodoma mara baada ya kukabidhiwa jengo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando akionesha funguo za Jengo la Kituo cha Mfano cha NHIF Dodoma mara baada ya kukabidhiwa jengo
 Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi
 Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma

 Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma Ujumbe wa NHIF na Hospitali ya Mkoa Mara baada ya kupokea Jengo
 

HABARI MOTORAIS AMSIMAMISHA KAZI KAMSHNA MKUU WA TRA


Rished Bade
Rais John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi  Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade na kumteua Dr Phillip Mpango kukaimu nafasi yake. Rais amemuagiza Bade kuhakikisha anamsaidia Dr Mpango kufanya kazi iliyoamriwa na Waziri Mkuu mapema leo.
Dr Phillip Mpango
Hatua hii kubwa Kitaifa imetokana na hatua ambazo zimechukuliwa na Waziri Mkuu mapema mchana wa leo. Mapema leo maafisa watano na watumishi watatu wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo wamesimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Khasim Majaliwa  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza leo mchana. Watu hao wamesimamishwa kwa tuhuma za  kusababishia serikali hasara ya Shilingi Bilioni 80, kutokana na kupotea kwa makonteina 369. Waliosimamishwa ni Kamishna wa Forodha  Tiagi Masamaki....si mara ya kwanza kusikia jina hili kwa kumbukumbu tu.....

Tiagi Masamaki
(Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Biashara na Viwanda imeitaka Bodi ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kutoa maelezo ya vigezo vilivyotumika kumpandisha cheo ofisa wake anayetuhumiwa kwa kushindwa kusimamia wajibu wake. Ofisa huyo Tiagi Masamaki, awali alikuwa Kaimu Kamishina wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, wakati huo akikabiliwa na tuhuma kadhaa ikiwamo makontena kupotea mikononi mwake.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa aliibua hoja hiyo.),Mkuu wa kituo cha huduma kwa wateja Habibu Mponezya, pia wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Harun Mpande, Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu Eliachi Mremana afisa mwingine ambaye kitengo chake hakikutajwa Hamis Ali Omari. Na Waziri Mkuu pia alitoa amri kuwa hawa wakamatwe na kuwa chini ya ulinzi wa Polisi ili kusaidia katika kuzipata na kuzirudisha serikalini fedha hizo zilizopotea. Pia aliamrisha Ananngisye Mtafya, Nsajigwa Mandengele, na Robert Nyoni kuhamishiwa Mkoani mara moja ili kupisha uchunguzi wa ufisadi huo. Waziri Mkuu pia alimuagiza Katibu Mkuu wa Hazina kupeleka wataalamu kutoka  Wakala wa Serikali Mtandao (e Goverment) ili kugaua mifumo ya mitandao na kuangalia wizi ulikuwa unafanywaje katika TRA.

Jumatatu, 23 Novemba 2015

MWAKALEBELA AKANUSHA KUFUTWA KWA KESI YAKE DHIDI YA MCHUNGAJI PETTER MSIGWA NA MKURUGEZI WA MANISPAA YA IRINGA.
 FREDRICK MWAKALEBELA AKIWA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM  WILAYA YA IRINGA MJINI WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
 BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOANI IRINGA WALIPOKUWA WANAWASIKILIZA FREDRICK MWAKALEBELA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM WILAYA YA IRINGA MJINI.


Chama cha mapinduzi wilaya ya iringa mjini kimekanusha kufutwa kwa kesi yao dhidi ya Mkurungenzi wa Manispaa ya Iringa mjini pamoja na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa. Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM wa wilaya ya Iringa Mjini Elisha Mwampashe amesema kuwa taarifa zilizosambaa sehemu mbalimbali sio za kweli.

“Nimekuwa nikipigiwa simu nyingi toka jana nikipewa taarifa kuwa kesi yetu imetupiliwa mbali na imeenea sana kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali ukweli ni kwamba kesi ya uchaguzi namba tano ya 2015 haijafutwa”alisema Elisha Mwampashe. Mwampashe ameongeza kuwa kesi hiyo bado haijapangiwa siku ya kusikilizwa wala kupangiwa jaji wa kuendesha kesi hiyo hivyo anashangaa kuaona taarifa zinazendelea kuenena mitaani
“Ifahamike kuwa Mahakamani kuna shauri la msingi  ambalo lilikuwa na kupinga matokeo, na kuna  shauri dogo  namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa likizungumziwa jana kwa lengo la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria kuruhusu kufanya hivyo” alisema Elisha Mwampashe.
Mwampashe amemalizia kwa kuwataka wananchi  na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwa na subira kwa kuwa haki yao ya msingi itapatikana mahakani na kuwasii wananchi wanaopotosha taarifa hizi waache mchezo huo.
Kwa upande wake Fredrick Mwakalebela aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini amesema kuwa shauri lilofutwa ni la kuomba kupunguziwa pesa ya dhamana.

“Nilikuwa kimya kutokana na kufatilia swala hili kimya kimya kwa lengo la kupata haki yangu ya msingi ambayo nimenyang’anywa na Mkurugezi wa Manispaa ya Iringa Mjini, pamoja na Mchungaji Peter Msingwa” alisema Fredrick Mwakalebela 

Mwakalebela amemalizia  kwa kusema kuwa kesi hiyo inaendeshwa naye pamoja na Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa chama ndicho kilichompa nafasi ya kugombea nafasi hiyo.

Mapema ilitolewa taarifa kuhusu kutupiliwa mbali kwa shauri ya dhamana ya kesi ya Ubunge Iringa Mjini.  Msajiri wa Mahakama kuu Iringa Bi Ruth Masamu amesema aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo La Iringa Mjini Fredrick Mwakalebela alitoa ombi la kuomba kupunguziwa dhamana kutoka milioni kumi na kushuka angalau kwa kiasi kidogo. Hii ni kutokana na vifungu vya sheria kuruhusu kuomba ombi hilo na mahakama kulikataa na kumtaka aongeze mtuhumiwa ambaye ni mwanasheria wa serikali kwenye kesi yake kwa gharama hiyohiyo. 

PICHA ZA KUMBUKUMBU BAADA YA RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KUZINDUA BUNGE DODOMA

IMGL0951 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wabunge muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL0959 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe Pius Msekwa huku Spika Mstaafu mwingine Mhe Anne Makinda akisubiri zamu yake muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL0963 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na mmoja wa wabunge muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL0969 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Benjamin William Mkapa muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL0970 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Benjamin William Mkapa muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL0973 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Benjamin William Mkapa muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL0977 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wakuu na wabunge muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL1021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza kwa unyenyekevu mawaidha toka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL1028 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL1046 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa wakijichanganya na wabunge kwenye mchapalo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL1061 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhe Zitto Kabwe muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL1121 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe Anthony Diallo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL1128 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Shadya Karume na MAma Khadija Mwinyi muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015IMGL1210 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wabunge na wageni waalikwa kwenye mchapalo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. Ni hapo alipoamuru kwamba zaidi ya shilingi milioni 200 zilizochangwa na wafadhili kwa ajili ya mchapalo huo zitumike kwa kununulia vitanda vya wagonja katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.IMGL1214 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti mwakilishi wa Benki kwa mchango wao kwenye mchapalo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015.IMGL1219 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio kwa mchango wao kwenye mchapalo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015.IMGL1221 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw.Adam Mayingu kwa mchango wao kwenye mchapalo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015.IMGL1227 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Mama Ineke Bussemaker kwa mchango wao kwenye mchapalo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015.IMGL1232 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti Mwakilishi wa NSSF kwa mchango wao kwenye mchapalo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015.IMGL1236 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru Spika Job Ndugai wakati anaondoka baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015.rwa4 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipozi na badhi ya mabalozi wa nchi za Kiafrika waliokaribishwa kwenye hafla ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015.

Ijumaa, 20 Novemba 2015

MSANII NILIVYOIPOKEA HOTUBA YA RAIS KUZINDUA BUNGE LA 11


FB_IMG_1438963514104-1
KWA MUDA MREFU wasanii wazalendo wengi tumekuwa tunakereketwa na mengi yaliyokuwa yanafanyika katika nchi hii dhidi ya wasanii na wabunifu. Watu wote duniani wana tamaduni zao. Kinachotofautisha taifa moja na jingine sio nguvu zao za kiuchumi, hilo hupimwa katika vipimo vya pato la nchi, uwezo wa kununua bidhaa au maendeleo yao ya kijamii. Hivyo ni vipimo tu vya kuonyesha uko ngazi gani katika dunia hii. Lakini katika swala la Utamaduni kila Taifa liko tofauti, hivyo kwa hilo wote tuko sawa, kwani ni kwa kupitia kigezo cha Utamaduni ndipo ambapo nasi tunasimama bila aibu kushindania na Taifa lolote duniani. Katika Taifa kama letu lenye makabila zaidi ya 120, pia kila kabila linatambulika kuwa sawa na jingine kutokana na tamaduni za kabila husika. Uwingi huu wa tamaduni ndogo (subculture) ni baraka kubwa kwa Taifa letu, baraka ambazo tunatakiwa tujifunze namna ya kuzilea na kuzithamini na kuzikuza, ili tuweze kuendelea kusimama kifua mbele tukiwa kama Taifa. Tusikosee na kuanza kujilinganisha na tamaduni nyingine, kwani kwa kuwa na tamaduni tofauti na nyingine ndio thamani kubwa ya utamaduni wetu. Kama Taifa ni muhimu kujali Utamaduni wetu, urithi wetu wa kiutamaduni, na wakati huohuo kuangalia wakati ujao na kujipanga kulea na kuendeleza Utamaduni wetu katika ulimwengu huu ambao sasa umekuwa kama kijiji. Kwa mtazamo huo basi wasanii ambao tumekuwa tukijua kazi nyingi na nzuri za sanaa zinatengenezwa Tanzania ZINGETUMIWA ipasavyo na Watanzania, zingeleta hali ya kujitambua , kujivunia Utanzania, na kuhakikisha ajira kwa Watanzania. Kuna mambo yalikuwa yana umiza roho sana , kwa mfano WIZARA katika serikali ya Tanzania kuagiza kundi la Makirikiri kutoka Botswana kwa ajili ya sherehe ya Wizara hiyo. Je, ni kweli hakuna vikundi Tanzania vinavyoweza kucheza ngoma mpaka hata ngoma za kiasili kuagiza Botswana? Balozi zetu zingetumia sanaa kutoka Tanzania, hakika zingekuwa na sura tofauti yenye utambulisha wa Tanzania, uamuzi huo ungewezesha wasanii wa Tanzania kupata kipato, ungesaidia wasanii kutambulika katika nchi ambazo kazi hizo zipo na kuchangia katika kukaribisha watalii nchini Tanzania. Uamuzi wa kutumia samani za Tanzania utahakikisha mafundi seremala wa Kitanzania wanapata ajira, kipato na wao kuchangia pato la nchi. Kutambuliwa kwa wasanii kama ni kundi maalumu katika hotuba ya Rais, kuna onyesha siku mpya katika kundi hili. Katika ripoti ya BASATA ya mwaka 2006, idadi ya wasanii nchini wakati huo ilikisiwa kuwa ni kiasi cha milioni sita. Kwa kuwa ni miaka tisa sasa imepita toka wakati wa ripoti hiyo kuna kila sababu ya kuamini kuwa kundi hilo limekuwa kubwa zaidi. Mara nyingi sana watu wengi hudhani wasanii ni wanamuziki na waigizaji tu, hiyo si kweli karibu kila nyumba nchini ina msanii, wasusi, wafinyanzi, wachoraji, waimbaji, na wasanii wengine wa aina mbalimbali ambao wengine maisha yao na familia zao hutegemea kazi zao za kisanii, kwa ukweli huu kila kijiji kina wasanii na hili ni kundi kubwa la watu. Ukitaja wafugaji, ndani yake kuna wasanii, ndani ya wakulima wamo wasanii, na kila kundi lina wasanii, na bada ya hapo kuna kundi kubwa la wanaohudumia wasanii au wanotegemea wasanii hawa au kazi zao ili waishi,watu kama wafanyakazi wa vyombo vya utangazaji, wafanya kazi katika biashara ya matangazo, wasambazaji, wafanya biashara ndogondogo, (machinga) na wengine wengi waliomo katika mnyororo wa biashara hii ikiwemo, maproducer, mameneja, mafundi mitambo, watayarishaji wa maonyesho na kadhalika. Hivyo sanaa si utamaduni tu bali ni kazi yenye nafasi kubwa ya ajira na mapato makubwa. Ripoti ya WIPO ya mwaka 2012 imeonyesha kuwa kazi zitokanazo na Hakimiliki huingiza mapato zaidi katika uchumi wa Taifa kuliko MADINI, jambo ambalo ni wazi wengi wanaosikia kwa mara ya kwanza hushangaa na hata kubisha, na hasa kwa kuwa kelele za mapato ya Madini ni kubwa sana katika jamii wakati hakuna anaelalamika kuhusu mapato kutokana na raslimali ya nchi inayoitwa sanaa. Ripoti hiyo ya WIPO pia ilionyesha kuwa sekta ya Hakimiliki inaajiri watu wengi zaidi kuliko, sekta za Madini, gesi, maji, Ustawi wa Jamii, Afya, Usafirishaji. Hivyo ni sekta ambayo ina umuhimu sana katika uchumi wa Taifa ikiwa italindwa inavyostahili. Hotuba ya Rais imeleta matumaini mapya katika tasnia ya Sanaa. 
 John Kitime

HAKIKA HATUKUKOSEA

sasa tufanye kazi, hakika hatukukosea kumpigia debe Rais John Pombe Magufuli

Jumanne, 17 Novemba 2015

WASIFU WA SPIKA WA JOB YUSTINO NDUGAI


Job Yustino Ndugai  alizaliwa tarehe 21 January  mwaka 1960. Alisoma katika shule ya msingi ya  Matare Primary School, na kisha kujiunga na sekondari ya Kibaha na A level alipata Old Moshi High School. Amepitia vyuo kama  Mweka College, University of Dar es Salaam, Agriculture University ya Norway na Open University ya Tanzania. Alipitia Jeshi la Kujenga Taifa kambi za Ruvu na Maramba. Amekuwa Mbunge wa jimbo la kongwa kuanzia mwaka 200o. Na kuanzia leo ndie spika wa Bunge La Jamhuri  kwa miaka mitano ijayo.

Ijumaa, 6 Novemba 2015

TNRF WAMTAKA MAGUFULI ADHIBITI UPOTEVU WA MALIASILI NCHINI


 Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) ,Dr.Suma Kaare akizungumza katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la Haki kazi Catalyst Alais Moridant akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la AWF ,John Salehe  akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Viongozi mbalimbali wa jumuiko la maliasili wakiwa katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja, ,mkutano huo ulihudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
Mwakilishi wa Shirika la WWF ,Sware Semesi  akizungumza katika  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
Wasemaji Wakuu wa   mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 

Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini Dr.Suma Kaare amemtaka Raisi John Pombe Magufuli adhibiti upotevu wa mali asili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.

Suma Kaare amesema  hayo katika mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  unaoendelea jijini Arusha,Kaare amesema kuwa jukwaa hilo litashirikiana na Rais huyo katika  kuhakikisha kuwa maliasili zinalindwa na kuwanufaisha Watanzania kwa kiwango stahiki.

“Tunajua Rais wetu mpya ana kazi  kubwa  ya kulinda maliasili za nchi hii kama ilivyo kauli mbiu yake ya “kazi tu” tunaamini atazuia upotevu mkubwa wa rasilimali unaofanywa na watendaji wasio waaminifu” Alisema Kaare

Mratibu wa Masuala ya misitu katika shirika la uhifadhi wa maliasili na Mazingira (wwf) ,Isaac Malungu amesema kuwa asilimia 90% ya nishati inayotumika nchini inatokana na kuni pamoja na mkaa hali ambayo inaathiri misitu na kutishia uhai wa maliasili nchini hivyo ameitaka serikali ihimize matumizi ya nishati mbadala ili kunusuru mazingira yanaoharibiwa kila kukicha.

Malungu alisema kuwa kilimo cha kuhama hama pamoja na ukataji miti ovyo umekua ukisababisha uharibifu wa mazingira na hata kupelekea hecta laki 4 za misitu kupotea kila mwaka kutokana na shughuli hizo.

Mkurugenzi wa  Shirika la AWF,John Salehe Alisema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha hali ya ukame inayowaathiri wanyama pamoja na mimea hivyo kuathiri uhifadhi kwa ujumla .

Salehe alisema kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo upandaji wa miti pamoja na kutunza misitu ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.

PICHA MBALIMBALI ZA SHEREHE ZA JANA ZILIZOSAMBAA KWENYE WHATSAPP