HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 27 Novemba 2015

HABARI MOTORAIS AMSIMAMISHA KAZI KAMSHNA MKUU WA TRA


Rished Bade
Rais John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi  Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade na kumteua Dr Phillip Mpango kukaimu nafasi yake. Rais amemuagiza Bade kuhakikisha anamsaidia Dr Mpango kufanya kazi iliyoamriwa na Waziri Mkuu mapema leo.
Dr Phillip Mpango
Hatua hii kubwa Kitaifa imetokana na hatua ambazo zimechukuliwa na Waziri Mkuu mapema mchana wa leo. Mapema leo maafisa watano na watumishi watatu wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo wamesimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Khasim Majaliwa  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza leo mchana. Watu hao wamesimamishwa kwa tuhuma za  kusababishia serikali hasara ya Shilingi Bilioni 80, kutokana na kupotea kwa makonteina 369. Waliosimamishwa ni Kamishna wa Forodha  Tiagi Masamaki....si mara ya kwanza kusikia jina hili kwa kumbukumbu tu.....

Tiagi Masamaki
(Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Biashara na Viwanda imeitaka Bodi ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kutoa maelezo ya vigezo vilivyotumika kumpandisha cheo ofisa wake anayetuhumiwa kwa kushindwa kusimamia wajibu wake. Ofisa huyo Tiagi Masamaki, awali alikuwa Kaimu Kamishina wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, wakati huo akikabiliwa na tuhuma kadhaa ikiwamo makontena kupotea mikononi mwake.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa aliibua hoja hiyo.),Mkuu wa kituo cha huduma kwa wateja Habibu Mponezya, pia wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Harun Mpande, Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu Eliachi Mremana afisa mwingine ambaye kitengo chake hakikutajwa Hamis Ali Omari. Na Waziri Mkuu pia alitoa amri kuwa hawa wakamatwe na kuwa chini ya ulinzi wa Polisi ili kusaidia katika kuzipata na kuzirudisha serikalini fedha hizo zilizopotea. Pia aliamrisha Ananngisye Mtafya, Nsajigwa Mandengele, na Robert Nyoni kuhamishiwa Mkoani mara moja ili kupisha uchunguzi wa ufisadi huo. Waziri Mkuu pia alimuagiza Katibu Mkuu wa Hazina kupeleka wataalamu kutoka  Wakala wa Serikali Mtandao (e Goverment) ili kugaua mifumo ya mitandao na kuangalia wizi ulikuwa unafanywaje katika TRA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni