HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 27 Novemba 2015

NHIF YAKABIDHIWA KITUO CHA MATIBABUCHA MFANO DODOMA


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika. Makadhiano hayo yamefanyika mjini Dodoma leo Ijumaa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa wa Dodoma na timu ya wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo kampuni ya Nosuto Associates. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando, amesema kukamilika kwa jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili kuanza kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi. Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF. Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji wa madai na utambuzi wa wagonjwa. Kaimu Mkurugenzi mkuu pia alisema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa. Naye Mkurugenzi wa fedha, mipango na uwekezaji wa NHIF Bw Desudedit Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania. Picha za kituoSehemu ya  mapokezi  ya kituo cha matibabu cha mfano cha NHIF Dodoma Sehemu ya mapokezi ya kituo cha matibabu cha mfano cha NHIF Dodoma
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando akionesha funguo za Jengo la Kituo cha Mfano cha NHIF Dodoma mara baada ya kukabidhiwa jengo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando akionesha funguo za Jengo la Kituo cha Mfano cha NHIF Dodoma mara baada ya kukabidhiwa jengo
 Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi
 Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma

 Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma Ujumbe wa NHIF na Hospitali ya Mkoa Mara baada ya kupokea Jengo
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni