HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 25 Machi 2015

ILI MBEGU IWEZE KUMEA LAZIMA IFE KWANZA


NIFAGILIE MPAKA NIWE PREZDA


GALAGALAA KWA AJILI YA CHAMA


2015 TUTASIKIA KILA AHADI


UNAFAHAMU BVR WEWE?

kwa zaidi ingia http://www.malickys.com/

NJOO NIFWATE TANZANIA KUEKTI TEA PARTY

CHAMA kipya kabisa nakianzisha next week. Kuna watu wameniudhi sana eti wameniwekea bifu, mimi siwekewagi bifu bwana mi nafanya kweli. Next week naanzisha chama langu la Kuekti. Yaani huko maigizo fulufulu, tutatengeneza muvi za ngumi, mieleka na kadhalika.
Karibuni ndugu zangu niungeni mkono mkono cham langu jipya Kuekti 2015. Kadi zinatolewa bila mashati samahani masharti. Huku profesa nanili kasema atajiunga, na yule nailino kasema atakuja na pia hata nanihii kasema atajiunga. Tuko fullu
Tanzania Kuekti Tea Party

WAMUANGUKIA SPIKA

Yaani mnamuangukia mama wa watu bila kosa, dahh aise wadau , vipi tena, akiumia mtampeleka nyinyi hospitali?

KIGOGO CHA CHAFULIWA

WATUwakorofi sana tena sana sana, wamediriki kukichafua kigogo kimoja pale mtaani kwetu. Kigogo hicho ambacho wote tulikuwa tukikitegemea kimechafuliwa kabisa, hivi saa hizi hamna mwenye shida na kigogo kile.

DARASA ZIMA WOTE MMEFELI

Hediticha wa shule moja kule Dom katangaza karibu shule nzima imefeli, baada ya darasa hilo kuwa katika shule hiyo kwa miaka mitano. Ticha huyo alitangaza last wiik kwa sauti kubwa, 'Asilimia 80 ya madent hamna kitu kabisaaaa'. Wananchi wanaoishi kando kando na shule walikuwa na haya ya kusema;
Mzee Kauzu-'Ehh ni kweli mimi mwenyewe nilikuwa nawaona wanacheza tu hata darasani wakiingia wanacheza tu ndio nikajisemea kimoyomoyo, hawa watafeli'
Mama Salome-'Ndio wamefeli, tena sio asilimia 80 tu hata huyo hediticha nae kafeli,watafelije asilimia 80 yeye abaki? wote wamefeli'
Denti -'Nani kafeli? Sisi wakali sana, yaani hebu fikiria tuna akili mpaka tunalala darasani, we usituchezee sisi'
Mpaka mtandao huu unaenda hewani ubishi ulikuwa unaendelea

WALA MIMI SIKUWAITA NASHANGAA

Yaani we acha tu. Mi nilikuwa niko sebuleni kwangu nimetulia, nakunywa chai yangu taratibu, sina neno na mtu, ghafla si nikasikia nje kuna kelele watu wamejaa mbele ya nyumba yangu. Nikashangaa sana, unajua mi ni mtu mpole sipendagi kelele, nikatoka nje nikashangaa kukuta eti watu kibao wamebeba mabango wanapiga kelele, "Wewe tu mzee wewe tu". Unajua siku hizi kuna mikasa mingi, nikajua sijui labda wananifananisha na jambazi. Mwili ukawa unatetemeka, nikawa nafikiria kukimbia. Ndio akajitokeza mzee mmoja wala simfahamu, akanambia, "Mkuu sisi wote tumeoteshwa kuwa unafaa kuwa mwenyekiti wetu wa serikali ya mtaa, hivyo tukajikuta tuu tumefika hapa kwako" Nilishangaa sana kwa upendo mkubwa wa hawa wanamtaa wenzangu, basi si unajua mi mpole ndio nikaona niwakubali kishingo upande. Nikasema," Kwa kweli mi sitaki hicho cheo lakini kwa kuwa mnanilazimisha, basi nikikipata ntawaletea kila nyumba chai maandazi kila siku, halafu ntahakikisha hakuna mtu anafanya tena dhambi mtaa huu. Wote tutaanza kuishi kama peponi' Ndio kishingo upande nikajisemea kimoyomoyo, "Ok ngoja niwe Mwenyekiti" Kuangalia kushoto kwa nyumba yangu nikapata shock, kumbe watoto wangu walikuwa wamekwisha wapangia viti wale wageni waliokuja ghafla, wakawa wamewawekea na matenti na chai na makeki, yaani mwenyewe nikashangaa. Basi ndio nikakaa na wananchi wenzangu nikala nao chakula cha mchana nikawapa nauli wakaondoka kurudi kwao kwa furaha.