HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Alhamisi, 21 Januari 2016

NHIF Yakabidhi Kadi za Matibabu kwa Wanachama wa Tanzania Bloggers Network


Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo.Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo.Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo.Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN.

NEWS ALERT: JPM AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Bwana Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bwana Piniel Mgonja   ili kupisha uchunguzi, kufuatia dosari alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.

RAIS POMBE MAGUFULI, AKIWA FUNDI CHEREHANI


 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es salaam Januari 20, 2016 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi wa hali ya juu
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.

Jumanne, 12 Januari 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA PERAMIHO


Waziri Ummy Mwalimu akisalimiana na Padri Lucius wa hospitali ya Peramiho Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Peramiho, Dr Venance Mushi, alipotembelea hospitali hiyo asubuhi ya leo Baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), wakiwa sehemu ya mapokezi, tayari kwa kupata huduma Mheshimiwa Ummy Mwalimu akiwafariji wagonjwa hospitalini hapo

Waziri Ummy Mwalimu Afanya Ziara ya Kikazi Kijijini Mpingi, Songea Vijijini na Kulikwamua Jengo la Zahanati lililokwama

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa  Bima ya Afya.
Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na
na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.
Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi
Baadhi ya wananchi wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri Ummy Mwalimu alipotembelea majengo ya zahanati yao

Waziri Ummy Mwalimu akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya,  kutembelea majengo ya zahanati ya Kijiji cha MpingiMzee Mohamed Mussa, mkazi wa kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kutembelea kijiji chao na kutoa msaada wa bati na misumari ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji

Jumatatu, 4 Januari 2016

KARIMJEE YAKABIDHI SCHOLARSHIP KWA WASHINDI WA SAYANSI 2015, WAPAA KWENDA IRELANDWanafunzi John Method (kushoto) na Edwin Luguku (wa pili kulia) kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe mkoani Morogoro wakipokea hati zao za ufadhili kutoka kwa Karimjee na Ofisa Ubalozi wa Ireland nchini, Bi. Carlo. Wanafunzi hao waliibuka washindi wa jumla katika maonesho ya Sayansi kwa Shule za Sekondari mwaka 2015 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST). (Picha zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).

Ofisa Ubalozi wa Ireland nchini, Bi. Carlo, akizungumza na Edwin Luguku na John Method kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro ambao waliibuka washindi wa jumla katika maonesho ya Sayansi kwa Shule za Sekondari mwaka 2015 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST). Wanafunzi hao wanaondoka leo hii kwenda Dublin, Ireland kwa maonesho ya sayansi.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Dk. Gozibert Kamugisha, akizungumza wakati wa kukabidhiwa kwa scholarship kwa wanafunzi Edwin Luguku na John Thomas wa Shule ya Sekondari Mzumbe ambao walikuwa washindi wa jumla katika maonesho ya sayansi 2015. Wanafunzi hao walipewa scholarship hizo la taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam.
Meneja wa taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation, Devota Rubama, akizungumza kabla ya kukabidhi hati za ufadhili kwa wanafunzi Edwin Luguku na John Thomas wa Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro walioshinda katika maonesho ya sayansi 2015.
Mzee Karimjee, Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation.

Toyota Tanzania Limited nao waliwazawadia vijana hao kwa ushindi walioupata.

Na Daniel Mbega
TAASISI ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam leo hii imekabidhi scholarship kwa wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro, ambao waliibuka washindi wa jumla katika Maonesho ya Tano ya Sayansi ya YST kwa Shule za Sekondari Tanzania Agosti 2015.
Wanafunzi hao, Edwin Luguku na John Method, ambao leo hii wanakwenda jijini Dublin, Ireland kuhudhuria Maonesho ya 53 ya Sayansi, waliibuka washindi kutokana na utafiti wao wa sayansi usemao “Madhara ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki Tanzania na Namna ya Kupunguza Matumizi hayo” (The Effects of Using Plastic Bags in Tanzania and How to Reduce the Same).
Kutokana na udhamini huo, wanafunzi hao wawili ambao wanatarajia kumaliza kidato cha sita mwaka huu, watasomeshwa na taasisi hiyo chuo kikuu huku wakilipiwa ada pamoja na gharama nyingine zote kwa miaka yote watakayokuwa wanachukua shahada zao.
Itakumbukwa kwamba, Taasisi ya Karimjee Jivanjee mbali ya kutoa scholarship kwa wanafunzi hao, pia ilitoa ufadhili kwa shahada ya kwanza chuo kikuu kwa wanafunzi Petro Samson Ndegeleki na Juma Joshua Wiliam kutoka Nassa Sekondari ya Simiyu ambao utafiti wao ulihusu ‘How Different Natural Fertilizers Affect the Growth Of Maize’.
Washindi hao pia wanaondoka leo hii kwenda Dublin, Ireland kuhudhuria maonesho ya sayansi ya 53 maarufu kama BT YSTE.
Aidha, taasisi hiyo, ambayo ilianza kudhamini maonesho hayo tangu mwaka 2012, pia iliwazawadia washindi wa pili wa jumla ambao ni Emmanuel Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling Ecto-parasites’.
Meneja wa taasisi hiyo, Devota Rubama, amesema kwamba taasisi hiyo imejikita katika kusaidia huduma za kijamii hususan elimu, ambapo kwa mwaka 2015 ilitenga kiasi cha Shs. 1 bilioni huku akiahidi kwamba, kwa mwaka 2016 wametenda Shs. 1.5 bilioni.
“Tumedhamiria kuwahamasisha wanasayansi chipukizi wa Tanzania ili kukuza vipaji vyao ili kulisaidia taifa,” alisema.
Akaongeza: “Tangu mwaka 2015 hadi sasa tumetoa ufadhili kwa wanafunzi 15 ambao walikuwa washindi wa jumla na kila mwaka hutoa ufadhili kwa wanafunzi wanne wanaoshinda katika maonesho ya YST. Wanafunzi walionufaika na ufadhili huo ni watatu kutoka Kibosho Sekondari (2012), wawili kutoka Ilongelo Sekondari, Singida na wawili kutoka Fidel Castro, Pemba (2013), wawili kutoka Lumumba Sekondari, Unguja na wawili kutoka Ngongo Sekondari, Lindi (2014) na sasa tunatoa kwa wawili kutoka Mzumbe na wawili Nasa, Simiyu walioshinda mwaka 2015.”
Rubama alisema kwamba taasisi yake ina mpango wa kuanzisha ufadhili wa shahada ya uzamili kuhusu Uhifadhi Afrika (African Conservation) katika Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland na Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, Arusha ambapo wanufaika watakuwa watatu kila mwaka ambao watasoma mihula miwili Glasgow na mihula nane watamalizia Chuo Kikuu cha Nelson Mandela.
“Taasisi imekwishaanza kutoa ufadhili kwa shahada ya uzamili ya udaktari kuhusu Paediatric Oncology katika Chuo Kikuu cha Muhimbili ambapo madaktari wawili walihitimu mwaka 2015 na mwingine atapatiwa ufadhili mwaka 2016.
Katika maonesho hayo ya 5 yaliyoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST) kwa mwaka 2015 yalishirikisha jumla ya shule 240 na walimu 120 kutoka shule 120 nchini kote ambapo zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washindi zikiwemo fedha taslimu, medali, vikombe, vifaa vya maabara pamoja na maktaba.
Dk. Gozibert Kamugisha, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa YST, ameishukuru taasisi hiyo pamoja na Serikali ya Ireland kupitia Shirika la Kimataifa la Misaada la Irish Aid na kuomba wadau wengine wajitokeze kufadhili maonesho hayo.


 (Imeandaliwa na www.brotherdanny.com)