HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatatu, 21 Novemba 2016

Benki ya AMANA yazindua Huduma ya Mikopo midogo midogo kwa wafanya Biashara Mbagala Jijini Dar es Salaam

Diwani wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es salaam Mh Abdala  Mtimika (Kushoto) Pamoja na Mkurugenzi wa Bank ya Amana nchini Dr Mosen Masoud wakikata utepe Kuashiria kuzinduliwa Rasmi kwa Huduma ya mikopo Midogo Midogo kwa wafanya biashara wa Mbagala Jijini Dar es salaam.uzinduzi huo umefanyika katika Tawi la Amana Mbagala (Picha zote na Vicent Macha wa Habari24 blog)
 Hatimaye wakazi wa mbagala wanaofanya Biashara ndogo ndogo wakiwemo wajasiriamali wamepata neema kubwa baada ya Bank ya AMANA kuzinduaa huduma yake mpya ya kutoa mikopo midogo midogo kwa wafanya biashara, huduma ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni miaka mitano Tangu kuanzishwa kwa Bank Hiyo.
Akizungumza na wanahabari na wananchi wa mbagala ambapo ndio uzinduzi huo umefanyika Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen Masoud amesema kuwa huduma hiyo imeanzishwa mahususi kwa kutambua hitajio kubwa katika jamii la wafanya biashara wadogo wadogo katika kupata mtaji ya kukuza biashara zao hivyo Bank ya Amana imeamua kuwainua wafanya biashara hao wadogo ili kuinuka kipato chao na kufikia kipato cha kati na hata kipato cha juu.


Amesema kuwa kupitia huduma hiyo Amana Bank inawawezesha wafanya biashara kwa kununua bidhaa wanazohitaji katika biashara zao na kuwauzia kwa bei nafuu kwa mkopo ambapo watarejesha kidogo kidogo katika muda ambao umewekwa katika utaratibu.
Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen Masoud akizungumza na wanahabari na wananchi waliofika katika uzinduzi huo 
Ameongeza kuwa wafanyabiashara sasa wana nafasi ya kukodishwa vifaa mbalimbali wanavyohitaji katika kuendesha biashara zao kwa kodi nafuu na mwishowe wanaweza wakanunua vifaa hivyo kwa Bei nafuu
Mkurugenzi huyo ameendelea kueleza kuwa kwa sasa Huduma hiyo ya mkopo imeanza kutolewa kwa wateja wake wanaotumia Tawi lao la Mbagala tu lakini kusudi lao ni kuhakikisha kuwa wanaendesha zoezi hiyo latika matawi yao yote nchini ambayo kwa sasa yapo matawi saba.
Diwani wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es salaam Mh Abdala  Mtimika Akizungumza 
Akizunguza wakati wa uzinduzi huo Mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa kata ya Kibondemaji Abdala Mtimika ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Temeke amesema kuwa Uzinduzi wa Huduma hiyo ya kutoa mikopo midogo modogo sasa imekuja wakati muafaka kipindi ambacho watanzania wengi wamekuwa wakilalamika kudorora kwa uchumi na pesa kupotea hivyo ni jukumu la wafanya biashara wa mbagala kutumia nafasi hiyo adhimi kuhakikisha kuwa wanapata mikopo hiyo na kuwekeza katika Biashara zao.
Wiki ya Huduma kwa wateja ikiendelea wateja mbalimbali wakipata Huduma katika Tawi la Benk hiyo Mbagala leo
Aidha Diwani huyo amewapongeza sana uongozi wa Bank ya Amana Tanzania kwa kuweza kuendesha Bank hiyo kwa usawa pamoja na kuwa imekuwa ikijulikana kuwa Ni Bank ya kiislam ila sio kweli kwani imekuwa ikitoa Huduma kwa watanzania wote bila kujali Dini zao pamoja na kuwa inatumia Taratibu za kiislam.
Wanahabari wakiwa katika hafla hiyo
Uzinduzi wa huduma hiyo umekwenda sambamba na uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa mteja ambapo bank hiyo imeanza kuadhimisha wiki hiyo leo ikiwa ni kuendelea kusherekea miaka Mitano ya Bank hiyo tangu ianze kutoa huduma za kibenk nchini Tanzania.

Alhamisi, 17 Novemba 2016

JK AWATUNUKU DIGRII WAHITIMU 1,179 CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE


 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha  Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii za awali.

Digrii walizotunukiwa ni Elimu ya Jamii na Ualimu (B.A.Ed.) wanafunzi 864, Elimu katika Elimu ya Jamii (B.E.D. Arts) wanafunzi 52, Elimu katika Sayansi (B.Ed. Science) wahitimu 73, Sayansi ya Ualimu (B.Sc.Ed.) wahitimu 190.(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG- 0754 264203)
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuwatunuku digrii ya awali ya elimu ya jamii  na ualimu  wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo jioni. Jumla ya wanafunzi 864 walitunukiwa digrii hiyo.
 wakivaa kofia zao
 Wakifurahi kwa kucheza muziki
 Ni shangwe na vigelegele
 Mhitimu Bora wa Kike akipatiwa zawadi
 Warda Jumanne akipatiwa zawadi ya kuwa mmoja wa wanafunzi Bora wa Kike
 Mwanafunzi Bora wa Jumla Haji Mohamed akionesha cheti chake
 Makamu Mkuu wa UDSM, akifurahi wakati wimbo wa kabila la Kihaya wa Akanana Kalile Kona ukipigwa wakati wa mahafali hayo
 Ni muziki kwa kwenda mbele Eva akipatiwa tuzo ya mwanafunzi bora wa kike
 Mwanafunzi Bora wa Kike Gaudencia Mwita akielekea kutuzwa zawadi maalumu ya Mkuu wa Chuo
 Mwanafunzi Bora wa Jumla wa Duce, Haji Mohamed akitoa hotuba ya shukrani kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu
 Dk. Kikwete akifurahia jambo na Ngumbullu
 JK akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo hixo
Wananchi wakiwa na kamera tayari kuwapiga picha ndugu zao walihitimu

Jumatatu, 14 Novemba 2016

UN DELEGATES TO VISIT UN SUPPORTED PROGRAMS IN DAR ES SALAAM DODOMA AND KIGOMA


The Nordic countries (Sweden, Norway, Denmark, Finland and Iceland) are key donors and partners of the United Nations system globally, regionally and at country level. In order to strengthen their collaboration with the United Nations in support of the Global Goals, and strategic development priorities of the Government of Tanzania, officials representing the five Nordic countries will be in the country during 14 -18 November, 2016.

The mission comes during the initial implementation stage of the UN Business Plan (UNDAP II) as well as the Five Year National Development Plan of Tanzania. The mission, comprising of 13 delegates from Nordic Ministries of Foreign Affairs and five delegates from UN offices in Nordic countries, is expected to visit some of the UN supported programmes in Dar es Salaam, Dodoma and Kigoma.

The mission is expected to meet with senior government officials, including the Vice President of Tanzania, and Minister of Foreign Affairs, and East African Cooperation. They are also expected to meet with the National Assembly Speaker and other regional leaders in the regions they visit.

While in Dar es Salaam, on November 14-15, the mission will meet with the senior UN officials, government counterparts, and representatives from CSO’s and NGO’s. They will also visit a Gender and Children Desk in the police station of Chang’ombe and PASADA, an organization dealing with HIV and AIDS. These visits will demonstrate support to ending gender-based violence and violence against children, and for people living with HIV and AIDS, and enhancing democratic governance through the rule of law.

In Dodoma on November 16, the mission will meet National Assembly Leadership, where the UN, through its agencies, has been supporting capacity building for the past five years. The visits will include a Youth Employment Programme, the Three Sisters Oil Mills Company Limited - the Kizota Food Warehouse and TASAF.

The last leg of the visit will be to the Refugee Camp in Kigoma, on Thursday 17 November. Accompanied by Government and UN Officials, the mission will visit Nyarugusu Refugee Camp in Kasulu to see the humanitarian refugee response led by the UN, as well to meet with women’s associations in their host communities supported by UN interventions.

Highlighting the importance of the mission, on behalf of the UN System in Tanzania, the UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez, stated that the Nordic countries have been key partners to the UN in development and humanitarian activities, and this has allowed the UN to be a partner of the United Republic of Tanzania in addressing pressing national priorities. He added that their visit to Tanzania comes at the right time when the UN and the Government have developed their five-year plans for eradicating poverty, addressing climate change and ensuring sustainable development. Mr. Rodriguez added, “We in the UN are very pleased with the Nordic countries’ support and their commitment in ensuring no one is left behind when it comes to development and humanitarian assistance”.

THE LATE MZEE RICHARD BINAGI IS LAID TO REST IN DAR ES SALAAM

Burial ceremony for the Late Richard Binagi (88), who died on Tuesday  November 8th, 2016 took place at his home in Kipunguni Dar es Salaam. Mr Binagi was a retired army officer 
Na BMG
JWTZ soldiers saluting the coffin of Richard Binagi


Guard of honour

Family members laying wreaths. In the picture Prof. Profesa Lloyd Binagi and his wife
Mzee Chacha Binagi and his wife laying wreaths on the grave
Mama Binagi
Zakaria Binagi and wife
Other family members laying flowers


Click here for Swahili version of the burial ceremony HAPA 

Alhamisi, 10 Novemba 2016

MATUKIO BUNGENI LEO

 Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya na Mbunge kutoka Barza la Wawakilishi Zanzibar, Machano wakiingia bungeni Dodoma leo.
 Naibu Spika, Dk. Tulia Akson akizungumza na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiku baada ya kusitisha Bunge kwa ajili ya mapumziko mchana wa leo.
 Wabunge wakijadiliana jambo walipokuwa wakiingia bungeni Dodoma
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata (kulia), akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalumu, Joyce Sokombi kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma
 Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kingwangalah akijibu maswali ya wabunge
 Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (kushoto) akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Oliva

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Mbunge  wa Newala Vijijini, George Mkuchika
 Wanafunzi wa Shule ya ADC NARCO ya wailayani Kongwa wakiwa bungeni Dodoma kuona mwenendo wa bunge hiloSpika wa Bunge, Job Ndugai akiwasihi wabunge kuwa na tabia ya kuheshimiana baada ya Mbunge wa Mbozi, Haonga kumwambia yeye amekula maharage gani kiasi kwamba hawaoni kuwapa nafasi ya kuchangia hoja wabunge wanaokaa nyuma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akitangaza bungeni, Dodoma, kutengua baadhi ya kanuni ili mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge, marehemu Samuel Sitta uingie bungeni leo kwa ajili ya kuagwa na wabunge. Kulia ni Mwansheria Mkuu wa Serikali, George Masaju.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mashariki, Kolimba (kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anjelina Mabula wakiingia bungeni

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG