HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatatu, 19 Desemba 2016

ELLISHA JAMES' NEW SONG REALEASE!!!

BEI YAKE IS A SWAHILI WORD FOR "ITS PRICE". THAT'S ELLISHA JAMES'S NEW RELEASE. ITS AN URBAN RAP MUSIC  TO ALERT THE YOUNGSTERS THAT EVERYTHING IN THIS WORLD HAS  A PRICE , NOT ONLY FOR MONEY CASE BUT IT ALSO DESCRIBES HARD WORK AND WHAT IT PAYS IN RETURN. : TO SUCCEED YOU NEED WORK HARD  AND IF YOU PAY HARD WORK SUCCESS IS YOURS FOR THE TAKING
produced by Daz naledge & mastered by Ambrose Dunga under  Dab muzik,Proper entertainment

here is the link to listen & download the song

Wyre Da Love Child has a new video out

Kevin Waire better known as Wyre Da Love Child is a Kenyan R&B and reggae musician from known from the some of the most popular groups in music history- Necessary Noize and East African Bashment Crew as well as a solo artist.
With four albums out, namely “Defination of a Love Child”, “10 Years Wiser”, “Re-Wyred” and he recently released “Lion” just to be sure of cementing his well founded legacy.
Giving something new this time the dancehall maestro teams up with popular turn table doctor DJ Protege to bring you this fire hit release,“Work and Play” the new song is a simple feel good track that this two musical geniuses have teamed up together to remind you to have fun after work.The video was shot in the US,Atlanta.
Produced by Dj Protege and the video directed by Morgan Cashboy Films based in Atlanta,US watch the video here

Jumanne, 13 Desemba 2016

RIPOTI TOKA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;-

1. Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi vikaoni.

Ili kuwa  na vikao vya Chama vyenye tija imeamuliwa kama ifuatavyo:-

a). Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158 kama  ifuatavyo:-

Wenyeviti wa Mikoa
Mikoa ya Bara           26x1                               =      26
Mikoa ya Zanzibar      6x1                              =          6

Wajumbe wa NEC wa Mikoa
 Mikoa ya Bara                      26x1         =        26
 Mikoa ya Zanzibar                    6x4         =        24
Wajumbe wa NEC wa Taifa
 Kutoka  Bara                                   =               15
 Kutoka  Zanzibar                           =               15

Nafasi za Mwenyekiti                    =                7

Wajumbe wa NEC wa Jumuiya
        UVCCM                                                =        5
        UWT                                                     =        5
        WAZAZI                                               =        5
Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni     =        5

Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM      =       1

Wajumbe wa  NEC kutoka BLW                     =       3

Katibu wa Kamati ya Wawakilishi                =       1

Wajumbe wa NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao
- Mwenyekiti wa CCM                  =       1
- Makamu Mwenyekiti (B)         =       1
-Makamu Mwenyekiti (Z)           =       1
- Makamu wa Rais                        =       1
-  Waziri Mkuu                               =       1
- Makamu wa Pili wa Rais (Z)   =       1
- Spika wa Bunge                          =       1
- Spika  wa  BLW                           =       1
- Mwenyekiti wa UWT                =       1
- Mwenyekiti wa WAZAZI          =       1
-Mwenyekiti wa UVCCM             =       1
- Katibu Mkuu – WAZAZI            =       1
- Katibu Mkuu – UWT                   =       1
- Katibu Mkuu – UVCCM              =       1
                                              Jumla:      158
#. Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vifanyike kila baada ya miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

b). Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati Kuu wawe 24 badala ya 34 kama ifuatavyo:-

Mwenyekiti wa CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Makamu Mwenyekiti wa CCM        (Zanzibar)
Makamu wa  Rais
Katibu Mkuu wa CCM
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM  (Zanzibar)
Waziri Mkuu
Makamu wa Pili wa Rais (Z)
Spika wa Bunge la Tanzania
Spika  wa BWL
Mwenyekiti  wa WAZAZI
Mwenyekiti  wa UWT
Mwenyekiti  wa UVCCM
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Organaizesheni
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Itikadi na Uenezi
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Uchumi na Fedha
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Wajumbe  watatu (3)  wa kuchaguliwa  na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania

Wajumbe watatu  (3) wa kuchaguliwa  na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar.

#. Vikao vya kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili vifanyike kila baada  ya miezi minne badala ya miezi miwili isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

c). Kwa ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa wajumbe  watatu ambao ni:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa         -       1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Mkoa        -       2

#. Vikao  vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Mkoa vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila  mwezi kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

d). Kwa upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wapunguzwe kwa kuwoandoa:-
 Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya    -       1
 Katibu wa Kamati ya Madiwani                   -       1
 Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)-  2
                                                                            Jumla:  4

#.Vikao  vya kawaida  vya Kamati ya Siasa ya Wilaya  vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila  mwezi isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

#. Muundo wa Wilaya za Chama uendane na muundo wa sasa wa Serikali.

Kata,Tawi na Shina
Idadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50  hadi 300.

Idadi ya kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301 hadi 1,000.
Hata hivyo idadi hii izingatie eneo la kijiografia na wingi wa wanachama katika eneo hilo.

Vikao vya kawaida vya  Kamati za Siasa  za  ngazi hizi viwe vinafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

#. Nafasi za Uongozi
Mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi  moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa Chama Toleo la 2012 kifungu cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:-
Mwenyekiti wa Tawi,Kijiji au Mitaa.
Mwenyekiti wa Kata/Wadi.
Mwenyekiti wa Jimbo, Wilaya na Mkoa.
Makatibu wa Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika.
Mbunge, Mwakilishi na Diwani.

#. Viongozi wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji badala yake waongoze na kusimamia shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni.

#.Vyeo ambavyo haviko kwenye Katiba
Vyeo  ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM haviruhusiwi katika Chama au Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali kama Wenyeviti wa ngazi mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k), Makamanda (UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote.

#. Uhakiki wa Wanachama wa CCM
Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wa CCM  na Jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu.   Uhakiki huu uendane na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki na kadi za CCM tu.

#. Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi
Jumuiya za CCM  zimetakiwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za Jumuiya ziendane na  matakwa ya Katiba ya CCM.

#.Uaendeshaji  wa shughuli zote za Jumuiya za Chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi).
Makatibu Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na Kamati Kuu  na  Manaibu Katibu Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

#. Wakati tukiendelea kubaki  na Bendera yenye rangi ya kijani na njano  na  alama ya jembe na nyundo, Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi.

#. Utumishi  katika  Chama na Jumuiya zake. Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za Watumishi wa Chama na Jumuiya zake.

Nafasi za Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya zitaondolewa na badala yake kazi zao zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya  za Chama wa Mikoa na Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa.  Utaratibu huu utakipunguzia Chama Cha Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa Chama na Jumuiya zake katika Mikoa na Wilaya.

#. Tathimini ya hali ya Kisiasa na  Uchaguzi wa    Zanzibar .
Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kuundwa kwa Kamati maalum ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar 2015.

# Mwenyekiti wa Kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari 2017, Mikoa na Wilaya ambazo hazijaleta taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti na Nidhamu kabla ya tarehe 30/01/2017.

#. Uhakiki wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi ukikamilika Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa mapema iwezekanavyo.

#. Maamuzi na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na Kanuni za Jumuiya  za Chama.

#. Kwa mambo yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya Katiba, Mkutano Mkuu utaandaliwa mapema mwakani na kutafakari na kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba.

Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.

#.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.
#. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi
#. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
#. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.

Imetolewa na:-

                                                        NAPE NNAUYE
                                             IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
                                                         13/12/2016

Jumatano, 7 Desemba 2016

MFUKO WA LAPF KWA MARA NYINGINE WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UTUNZANI WA MAHESABU NCHINI

Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida (katikati mwenye tuzo), akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kutunukiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hutuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno.
 
 Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi NBAA. Profesa Isaya Jairo.
 Wapiga picha za habari wakiwa tayari kwa kazi.
 Wafanyakazi wa Mfuko wa LAPF wakipita meza kuu baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa NBAA.

Na Dotto Mwaibale

MFUKO wa Pensheni wa LAPF, umetunukiwa tuzo ya kuwa kinara katika utunzaji  wa mahesabu dhidi ya mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Elyudi Sanga baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa mfuko huo, John Kida, alisema kwao ni mafanikio makubwa kwa kupata tuzo hiyo. "Tunatumia njia za kisasa ya utunzaji wa mahesabu huku tukifunga mahesabu yetu kwa wakati jambo linalotupa fursa ya kuweka sawa mambo yetu ya mahesabu" alisema Kida. Alisema wamekuwa wakifunga mahesabu yao kwa kiwango cha kimataifa ndio maana wamekuwa wakiibuka washindi mara nyingi. Kida alisema kuwa ushindi huo ni wa mara ya nane tangu kuanzishwa kwa utoaji wa tuzo hizo mwaka 2008. Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe, alisema kuwa wanachama wao wanatakiwa kuendelea kuwa na imani na mfuko wao na kuwa fedha zao zipo kwenye mikono salama. Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Pius Maneno, alisema makampuni na taasisi 56 zilishiriki katika mashindano hayo kwa  mwaka huu ambapo waligawanywa katika makundi 12 kulingana na huduma wanazozitoa. Alisema tuzo hizo zina lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji katika suala zima la mahesabu na kuhakikisha viwanago vya kimataifa vinazingatiwa katika utunzaji wa mahesabu.
Aliwataka wahasibu nchini kuandaa taarifa bora za fedha ili kuboresha hesabu za mashirika na makampuni na kuongeza uwazi katika shughuli zao. Tuzo hizo ziliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) na zilitolewa juzi katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (ACP) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

SERIKALI YAITAMBUA UWEPO NA UMUHIMU WA BLOGGERS KAATIKA KUENEZA HABARI


Waziri akiingia ukumbini

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nauye, jana jioni alifunga rasmi Mkutano wa Tanzania Bloggers Network (TBN), mkutano ulioandamana na semina za mambo mbalimbali yanayohusu kazi na fursa katika blogging. Bloggers kutoka kila kona ya nchi walikutana katika ukumbi wa PSPF kwa siku mbili na kuweza kubadilishana mawazo na hatimae kutengeneza kamati mbalimbali ambazo zingeonesha mwelekeo wa TBN katika kuingia 2017. katika hotuba yake Mhe Nape alieleza kuhusu nguvu ya blogs wakati wa uchaguzi na na pia kueleza kuwa serikali inatambua uwepo na umuhimu wa blogs. Katika kuanza kutengeneza kanuni za sheria mpya ya vyombo vya habari, Mheshimiwa Waziri aliahidi kuangalia nafasi za blogs katika sheria hizo. Ufungaji wa mkutano huo ulinogeshwa na shamra shamra za kusherehekea mwaka mmoja wa Pamoja Blog.


Selfie na Waziri 1

Selfie na Waziri 2

Selfie na Waziri 3

Waendeshaji wamitandao ya kijamii (bloggers) wakipiga picha ya Selfie kadhaa na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mara baada ya kufunga  mkutano mkuu wa mwaka wa Tanzania Network (TBN) jijini Dar es Salaam jana

LAPF YAPATA TUZO YA USHINDI YA KWANZA KWA UFUNGAJI BORA WA MAHESABU YA MFUKO KWA MWAKA 2014/15


Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akipokea Tuzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Eliud Sanga  wa ufungaji bora wa mahesabu kwa mwaka 2015 kutoka kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. Shogolo Msangi. LAPF iliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo.

Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida aliyeshikilia Tuzo katika picha ya pamoja na watumishi wa Mfuko mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya ushindi wa kwanza ya Ufungaji bora wa mahesabu ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2014/15. Hafla ya kukabishi tuzo hizo zilifanyika tarehe 03/12/2016 jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko Bw. John Kida akiwa ameshikilia Tuzo, pamoja nae  ni timu ya Kurugenzi ya Fedha ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo ilifanikisha ushindi huo wa ufungaji bora wa mahesabu kwa mwaka wa fedha 2014/15 LAPF imekuwa mshindi wa kwanza mara  sita kati ya mara nane tangu kuanzishwa kwa Tuzo hizo zilizoasisiwa na NBAA mwaka 2008.


Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Pro. Isaya Jairo kwa ushindi wa kwanza wa ufungaji bora wa mahesabu ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2014/15. Tuzo hizo zilitolewa tarehe 03 Disemba, 2016.

Jumapili, 4 Desemba 2016

LAPF DONATES IRRIGATION EQUIPMENT TO A GROUP OF THE DISABLED IN BUIGIRI DODOMA


The Local Authority Pension Fund's (LAPF) Senior Marketing Officer, Rehema Makamba, donated on behalf of the authority, irrigation equipment to a group of disabled residents of Buigiri Village. It is expected that the equipment will help the group in the running of their vegetable farming project
Rehema Makamba (right) donating watering hose, part of irrigation equipment for the disabled in Buigiri