HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 7 Desemba 2016

LAPF YAPATA TUZO YA USHINDI YA KWANZA KWA UFUNGAJI BORA WA MAHESABU YA MFUKO KWA MWAKA 2014/15


Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akipokea Tuzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Eliud Sanga  wa ufungaji bora wa mahesabu kwa mwaka 2015 kutoka kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. Shogolo Msangi. LAPF iliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo.

Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida aliyeshikilia Tuzo katika picha ya pamoja na watumishi wa Mfuko mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya ushindi wa kwanza ya Ufungaji bora wa mahesabu ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2014/15. Hafla ya kukabishi tuzo hizo zilifanyika tarehe 03/12/2016 jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko Bw. John Kida akiwa ameshikilia Tuzo, pamoja nae  ni timu ya Kurugenzi ya Fedha ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo ilifanikisha ushindi huo wa ufungaji bora wa mahesabu kwa mwaka wa fedha 2014/15 LAPF imekuwa mshindi wa kwanza mara  sita kati ya mara nane tangu kuanzishwa kwa Tuzo hizo zilizoasisiwa na NBAA mwaka 2008.


Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Pro. Isaya Jairo kwa ushindi wa kwanza wa ufungaji bora wa mahesabu ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2014/15. Tuzo hizo zilitolewa tarehe 03 Disemba, 2016.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni