HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 7 Desemba 2016

SERIKALI YAITAMBUA UWEPO NA UMUHIMU WA BLOGGERS KAATIKA KUENEZA HABARI


Waziri akiingia ukumbini

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nauye, jana jioni alifunga rasmi Mkutano wa Tanzania Bloggers Network (TBN), mkutano ulioandamana na semina za mambo mbalimbali yanayohusu kazi na fursa katika blogging. Bloggers kutoka kila kona ya nchi walikutana katika ukumbi wa PSPF kwa siku mbili na kuweza kubadilishana mawazo na hatimae kutengeneza kamati mbalimbali ambazo zingeonesha mwelekeo wa TBN katika kuingia 2017. katika hotuba yake Mhe Nape alieleza kuhusu nguvu ya blogs wakati wa uchaguzi na na pia kueleza kuwa serikali inatambua uwepo na umuhimu wa blogs. Katika kuanza kutengeneza kanuni za sheria mpya ya vyombo vya habari, Mheshimiwa Waziri aliahidi kuangalia nafasi za blogs katika sheria hizo. Ufungaji wa mkutano huo ulinogeshwa na shamra shamra za kusherehekea mwaka mmoja wa Pamoja Blog.


Selfie na Waziri 1

Selfie na Waziri 2

Selfie na Waziri 3

Waendeshaji wamitandao ya kijamii (bloggers) wakipiga picha ya Selfie kadhaa na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mara baada ya kufunga  mkutano mkuu wa mwaka wa Tanzania Network (TBN) jijini Dar es Salaam jana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni