HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumamosi, 6 Februari 2016

PESA ZA FAINI ZINAZOKUSANYWA NA TRAFIK VISIGA ZINAISHIA WAPI?


Kituo cha Polisi cha Mlandizi, wilayani Kibaha, Pwani.


Na Mwandishi Wetu

ASKARI wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani, Kituo cha Polisi Mlandizi wamewasotesha kwa takribani masaa mawili  na nusu wanahabari kupata risiti ya malipo ya faini aliyotozwa dereva wao baada ya kudaiwa kufanya kosa la kutaka kulipita gari lingine sehemu isiyoruhusiwa.
Sakata hilo lilianza wakati polisi alipolisimamisha gari hilo katika Kituo cha Visiga, Mlandizi, wilayani Kibaha, Pwani ambapo alimuomba dereva leseni yake na kumuamuru ateremke ili ajieleze akiwa nje ya gari na hatimaye kumlipisha faini ya sh. 30,000 kwa kosa hilo.
Baada ya wanahabari waliokuwa kwenye gari hilo kumsubiri dereva kwa takribani nusu saa, waliamua kuteremka kumfuata kujua kinachoendelea, kwani walikuwa wana haraka ya kufika Dodoma muda waliopangiwa  ili waungane na msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda Singida kwenye
maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM. Lakini baada ya mmoja wao kuwauliza Trafiki sababu zinazosababisha kutomwachia dereva, walijibu kwa kashfa na kejeli, wakihoji kwani nyie ni akina nani? na dereva wenu asipolipa faini basi watakaa hapo kituoni hadi jioni. Mmoja wa wanahabari hao alilipa faini ya sh. 30,000 na kuomba risiti. Hapo ndo songombingo ilianza ambapo Trafiki wa kike alijibu kuwa  hawana risti bali kinachofanyika pale ni kuandikiwa tu taarifa ya kosa lao na kwenda Kituo cha Polisi cha Mlandizi kilichopo takribani umbali wa Km 5, na wengine waliokamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani waliamuliwa kwenda kupata risiti katika kituo hicho. Mabishano makubwa yalitokea hapo baina ya Trafiki na wanahabari waliokuwa wanahoji ni kwa nini kitabu cha risiti wala mashine za kielekroniki havipo hapo
ili kurahisisha kazi. Askari wa kike na mmoja wa kiume walijibu kuwa wasifundishwe kazi. "Msitupotezee muda hapa, nendeni Mlandizi, mkapate hiyo risiti,"alisema trafiki wa kike. Wakati anasema hivyo kumbe mhasibu wao alikuwepo palepale Visiga,
lakini bila kuwaambia ondokeni naye ili akawahudumie."
Pia, mmoja wa Trafiki aliuponda sana utaratibu wa wakosaji kulipia faini kwa kutumia mashine za elekroniki akidai kwamba ni hasara kwa trafiki na madereva ni bora mashine hizo ziishie Dar es Salaam zisipelekwe Mkoa wa Pwani. Trafiki wengine walisikika wakisema kuwa hivi hawa jamaa wanaolazimisha kupewa risiti ni akina nani, waache waende zao, wakafie mbali.
Maneno hayo yalionekana kuwaudhi wanahabari na kuamua kuondoka kwenda Kituo cha Polisi Mlandizi, kufuatilia risiti, lakini walichokikuta huko ni maajabu, hasa ya kuambiwa kuwa Mhasibu hayupo ofisini kwake amekwenda kununua peni.
Baada ya wanahabari hao kusubiri kwa takribani saa moja, waliamua kwenda kaunta kuulizia na kuomba kuzungumza na Mkuu wa Kituo ili awasaidie kupata risiti wawahi kwenda Dodoma, lakini mmoja wa askari aliyekuwa zamu aliwajibu
kuwa Mkuu wa Kituo hajafika ofisini amepitia Kibaha Mjini kwenye mkutano.
Alipoombwa awasaidie kumpata mhasibu, askari huyo alitoka nje hadi ofisi ya Mhasibu alipomkosa akaamua kumpigia simu na kuwajibu kuwa ametoka mara moja kwenda kununua peni. Jambo hilo liliwashangaza sana wanahabari na kuanza kuhoji kwamba iweje kitendo cha kununua peni  kitumie muda wote huo na kusababisha watu wakiwemo wao kukosa huduma tena asubuhi majira ya saa 3?
Mmoja wa wananchi aliyekwenda kituoni kupata huduma ya risiti, alisikika akilalamika kuwa tabia hiyo ya kuchelewesha kutoa huduma ipo sana kituoni hapo na kwamba wanaoonekana kabisa hawaendani na kasi ya kufanya kazi anayoitaka Rais Dk  John Magufuli ya 'Hapa Kazi Tu'.
Mle ndani ya Kituo cha Polisi walisikika wakiulizana kwamba hivi hawa watu wanaowasumbua na kutaka kuzungumza na mkuu wa kituo ni akina nani hawa, eti wanataka risiti, ebu tumpigie simu mhasibu aje atuondolee balaa hapa.
Baada ya muda askari mwenye E 3275 alitoka nje na kuwaambia wanahabari kuwa mhasibu amepigiwa simu atakuja muda si mrefu mhudumiwe muondoke, lakini mmoja wa wanahabari hao anayemiliki blogu ya Full Shangwe, John Bukuku,  alihoji kuwa hivi ni kwanini polisi wa kituo hicho hawaendani na kasi ya Rais Dk. Magufuli? alijibu kuwa kwani kuna nini? Baada ya muda Mhasibu aliwasili kwa Bodaboda, na alipofika aliwakebehi
wanahabari kwamba anawashangaa kwa yeye kumuacha kule Visiga alikokuwa nao na kuwahi kituoni, ndipo wanahabari nao wakashangaa kumuona tena kituoni hapo wakati wlipofika kituoni waliambiwa ameenda kununua peni.
Dereva alimwambia haya twende ukachukue risiti yako muondoke na watu wako. Dereva aliingia na kupatiwa risiti kutoka kwenye kitabu kipya ambacho kwa mujibu wa dereva kilionekana dhahiri kuwa ni kipya. Lakini kwa masaa yote waliyokaa wanahabari kituoni hapo (takribani masaa
mawili), hawakuwaona madereva wa magari waliokamatwa pamoja na gari lao na kuandikiwa makosa na faini pale Visiga, hawakufika Kituo cha Polisi kupatiwa risiti, kitendo ambacho kinaashiria fedha wanazolipishwa madereva kwa kutenda makosa hazitolewi risiti, hivyo mapato ya serikali kupotelea mifukoni mwa baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani.
Baada ya wanahabari hao kupata risiti majira ya saa 4:15 waliamua kuondoka kituoni hapo kuanza safari ya kwenda Dodoma kuwahi msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana uliokuwa unawasubiri kwenda Singida.MIAKA 39 YA CCM, MAKADA WATULIE NDANI YA CHAMA


Dinah Somba Samanyi ambae ni Katibu wa Wazazi (CCM) Mkoani Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Ikiwa hii leo ni Maadhimisho ya Miaka 39 tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM, Wanachama wake wametakiwa kutulia ndani ya Chama hicho badala ya kujitoa katika chama jambo ambalo huwafanya baadae kujutia.

Kauli hiyo imetolewa Mkoani Mwanza na Katibu wa Wazazi wa Chama hicho Ndg.Dinah Somba Samanyi, wakati akizungumza na BMG, kuhusiana na maadhimisho ya miaka 39 ya CCM mwaka huu 2016.

Samanyi ametanabaisha kwamba, mwaka huu ikiwa ni miaka 39 tangu CCM kuasisiwa February 05,1977 ikiwa ni baada ya Muungano wa wa vyama viwili vya ASP kutoka Zanzibar na TANU kutoka Tanganyika, ni vyema wanachama wake wakawa waadilifu na kuepukana na tabia zisizo za kimaadili ambazo ni pamoja na kujitoa ndani ya chama hicho kama ambavyo baadhi yao wameshuhudiwa wakifanya jambo ambalo hata hivyo huwafanya baadae kulijutia.

Kuhusu maadhimisho amesema "Chama kimejipanga vizuri katika kuadhimisha Siku hii na tangu kuzinduliwa Kitaifa kwa sherehe za maadhimisho haya kule Zanzibar, kumekuwa na shughuli mbalimbali zinazolenga kuimarisha uhai wa chama pamoja na kushiriki shughuli tofauti tofauti za kijamii".

Samanyi amebainisha "Katika Mkoani Mwanza kila Wilaya imepewa fursa ya kuandaa shughuli mbalimbali kwa ajili ya maadhimisho haya. Jumuiya mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya Wazazi zimeshiriki shughuli tofauti tofauti kama vile kutembelea mashuleni, kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutembelea wagonjwa Mahospitalini".

Nao baadhi ya makada wa vyama vya siasa Mkoani Mwanza wametoa maoni yao kuhusiana na miaka 39 ya CCM kikiwa ni chama kinachoongoza Serikali, ambapo Kada wa CCM Sarah Ramadhan anasema anasema kuwa miaka 39 ya chama hicho, taifa limepiga hatua kubwa kimaendeleo ikilinganishwa na miaka iliyopita huku Amos Joseph ambae ni Kada ya Chadema akisema kuwa miaka 39 ya uongozi wa CCM taifa limeshindwa kutatua changamoto za kimaendeleo ikizingatiwa kwamba maendeleo yaliyopatikana hayaendani na raslimali za asili zilizopo nchini.

Pengine Maoni ya Makada hao ni fursa nyingine ya kuiwezesha CCM kuzidi kuwatumikia vyema Watanzania ili miaka 40 ijayo mwakani kusiwepo na utofauti wa kimtizamo pindi makada wa vyama vya siasa watakapokuwa wakitoa tena maoni yao.

Kitaifa Sherehe za Miaka 39 ya Kuasisiwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka huu, zilizinduliwa Visiwani Zanzibar na Dkt.Ali Mohamed Shein ambae ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na kilele chake kinahitimishwa Mjini Singida katika Uwanja wa Namfua ambapo zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. 

Jumanne, 2 Februari 2016

WATUMISHI WA SERIKALI WACHELEWAJI KUENDELEA KUFUNGIWA MAGETI


IMG_0652

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Serikali haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za walipa kodi hususani wa kipatao cha chini.

  Hayo yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo.

Dkt. Kigwangalla alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.

“Serikali haitowavumilia watumishi wazembe, hivyo tutaendelea kuwafungia mageti na kuwashughulikia wale wazembe, tunataka watumishi wa umma wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi, mtumishi akizembea tutamtumbua majipu, akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu,” alisema Dkt. Kigwangalla.

Aidha alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza ahadi zote za ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.

“Hatutomuonea mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya ya mwaka 2015 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi,” alisema naibu waziri.

Hata hivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na hakuna michango yoyote.

“Natoa wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za kuendeshea shule hizo,” alieleza Dkt. Kigwangalla.

Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama watagundulika ni majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kiini kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma.