ON STAGE

FORD TANZANIA FACEBOOK

Jumamosi, 27 Mei 2017

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA AKABIDHIWA MWENGE WA UHURU UKITOKEA MKOANI LINDI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi (Kulia) katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi wakijadili jambo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kulia) wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Muonekano wa Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam ukitokea Mkoani Lindi.
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda, leo Mei 27, 2017 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi katika dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la shule ya msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma na baada ya hapo kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke tayari kwa kumulika miradi ya Maendeleo.

Mara baada ya kukagua Miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Temeke Mwenge wa Uhuru utazuru katika Wilaya ya Kigamboni tarehe 28/05/2017, Siku ya tarehe 29/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala, tarehe 30/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni na tarehe 31/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ubungo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa Mwenge wa uhuru ni chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961, ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika hivyo kuzuru katika Mkoa wa Dar es salaam itakuwa ni kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, Uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu.

Mhe Makonda alisema kuwa mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali kutokana na mabadiliko ya kidemokrasia baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Mhe Makonda alisema kuwa jitihada ya kudhibiti kusambazwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya ni kuifanya kuwa ajenda muhimu kiutekelezeji kwa mustakabali wa maisha ya watanzania kwa kuwa jambo hilo linagusa nguvu kazi ya Taifa.

Rc Makonda amebainisha kuwa jumla ya miradi 40 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam ikiwa na  thamani ya shilingi Bilioni 244,392,530,334 ambapo miradi 12 itazinduliwa, miradi 15 itawekewa mawe ya msingi, miradi miwili itafunguliwa na miradi 11 itatembelewa.

Mhe Makonda amewapongeza wananchi wa Mkoa wa  Dar es salaam kwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili huku akitoa wito kwa wakazi wa Manispaa ya Temeke, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote utakapozuru kwani pamoja na mambo yote Mwenge wa Uhuru ni urithi na nembo ya umoja katika maendeleo yetu.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa weledi wake katika utendaji hususani katika kudumisha amani na kuchagiza ukuzaji wa uchumi wa nchi kwa kutilia msisitizo uwajibikaji serikalini, kukemea wizi na ubadhilifu wa mali za umma sambamba na mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Mhe Zambi alisema kuwa wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli katika mapambano dhidi ya wizi wa mali za Watanzania hususani vita  ya kiuchumi aliyoianza hivi karibuni kwa kuzuia mchanga wa dhahabu kusafirishwa kwenda nje ya nchi. 

Mhe Zambi ametoa pongezi hizo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli mara baada ya kupokea Ripoti ya kamati iliyokuwa inachunguza hatma ya mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Magufuli Machi 29 mwaka huu ikiwajumuisha Profesa Abdulkarim Hamisi Mruma (Mwenyekiti), Profesa Justiania Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dokta Yusuph Ngenya, Dokta Joseph Yoweza Phili, Dokta Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.

Mwenge wa Uhuru utamaliza mbio zake mkoani Dar es salaam siku ya tarehe 31/05/2017 na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani siku ya tarehe 01/06/2017 katika Uwanja wa kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kuelekea Mafia Mkoani Pwani.

Ijumaa, 26 Mei 2017

MAGAZETI LEO 27 MAY 2017


AFRIKA SIYO MASIKINI, AFRIKA INAIBIWA


MAKALA HII IMETAFSIRIWA KUTOKA KWENYE MAKALA ILIYOANDIKWA NA Nick Dearden ni Mkurugenzi wa taasisi ya Uingereza ya  Global Justice Now. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa  Jubilee Debt Campaign.

Afrika si masikini, lakini tunaweza kuwasaidia watu wake. Ni ujumbe rahisi unaorudiwa katika maelfu ya picha, habari katika magazeti, na wakati wa maombi ya michango ya kupeleka Afrika kila mwaka, kwa sababu hiyo jambo hilo hatimae linaanza kuchukua nafasi ya ukweli.

Tukisoma tena na tena ujumbe huo , tunazidi kuhakiki ukweli kuhusu hadithi ambazo tumekuwa tukizisikia kuhusu Afrika maisha yetu yote. Picha tuliyonayo ya Afrika inazidi kuwa ya kweli.

Hebu tujaribu kupata ujumbe tofauti.

Afrika ni tajiri lakini tunaiibia mali yake. Ujumbe unakuwa kama uwongo, lakini ujumbe huu ndio mwelekeo wa ripoti  (pdf) iliyotayarishwa na vikundi vya kiharakati mbalimbali iliyotolewa hivi karibuni. Ripoti hii ikiwa imejikita na takwimu inaonyesha kuwa nchi za Afrika kusini mwa Sahara zina deni la zaidi ya $41bn.   
Ni kweli kuna fedha za zinazoingia katika nchi hizi kutoka nchi za nje, kiasi cha  $161bn  kwa mwaka, lakini fedha hizi ni mikopo, fedha zinazotumwa na wananchi wa nchi hizi wanaofanya kazi nchi za nje, na misaada mbalimbali. Lakini wakati huohuo kuna kuna kiasi cha $203bn kinahamishwa kutoka nchi hizi, kati ya hizo $68bn zikiwa ni pesa kutokana na kukwepa kodi. Makampuni ya kimataifa ‘huiba’ hizi fedha 'kihalali',  kwa kudai kuwa wao hupata faida yao kutokana na kuzihifadhi katika nchi zenye unafuu wa kodi na sio Afrika. Taratibu hizi zinazoitwa "illicit financial flows" huchukua kiasi cha asilimia 6.1 ya pato  (GDP) lote la bara la Afrika, au ni sawa na mara tatu ya misaada ambayo Afrika hupewa. Baada ya hapo kuna $30bn ambayo makampuni ya kimataifa huhamisha kutoka Afrika kwenda kwao kama faida ambazo kampuni hizi hupata kutokana na shughuli zinazofanya Afrika. Jiji la London limefurika na faida zilizokamuliwa kutoka kwenye ardhi na nguvukazi za Afrika. 
Kuna njia nyingi ambazo hutumika kukamua utajiri wa Afrika. Ukataji miti usio halali, uvuvi haramu, na biashara haramu ya wanyamapori unakamua $29bn  kwa mwaka. Hasara nyingine ya $36bn huingizwa kila mwaka kutokana na uharibifu unaoleta mabadiliko hasi ya tabianchi. Pamoja na kuwa uharibifu mkubwa mazingira ulioko Ulaya haufanywi na Waafrika lakini bila shaka matokeo ya mabadiliko ya tabianchi yatawaathiri Waafrika zaidi. Na hakuna mpango wowote wa kufidia hali hiyo.
Kiukweli hata kama kungekuwa na malipo yanayopelekwa Afrika, utafiti unaonyesha kuwa mtizamo uliopo kuwa misaada inayoingia Afrika inawanuafaisha watu wa bara hilo, si kweli kwani mikopo inayochukuliwa na serikali na taasisi binafsi, ambayo ni zaidi ya  $50bn huishia kuwa madeni yasiyolipika. Nchi ya Ghana inapoteza asilimia 30 ya mapato ya serikali kulipia madeni, madeni yaliyotokana na miradi ambayo haikutekelezeka, ambayo ilikuwa na riba kubwa kupindukia. Kwa mfano Msumbiji iliwahi kuchukua mkopo wa kujengwa mtambo wa kuyeyusha alumini, kwa sasa mtambo huo unaigharimu serikali ya Msumbiji  £21 kwa kila  £1 ambayo serikali ya Msumbiji inapata. Msaada wa Uingereza (British aid), unaotumika kuanzisha shule na hospitali za kulipia za binafsi, zinasababisha kupunguza kwa kasi ya kutengeza hospitali na shule za umma nzuri, jambo ambalo limeanza kusababisha shule za namna hiyo kuanza kufungwa Uganda na Kenya.  Lakini katika mazingira haya haya kuna Waafrika ambao wanatajirika sana. Takwimu zinaonyesha kwa sasa kuna Waafrika kiasi cha 165,000 ambao ni matajiri sana, kwa pamoja wanautajiri wa $860bn. Lakini kwa jinsi uchumi unavyofanya kazi matajiri hawa fedha zao hawaziweki Afrika, wameziweka katika nchi zile ziitwazo ‘tax havens’. 2014 kulikuwa na makisikio kuwa Waafrika hawa matajiri wana kiasi cha $500bn wameziweka katika benki za ‘tax havens’.  Watu wa Afrika wanaibiwa utajiri wao na aina ya uchumi ambao unawawezesha watu wachache kutajirika na hatimae kuhamisha uchumi huo kutoka Afrika.

Sasa nini kifanyike?  Nchi za magharibi hujinasibu kuwa ni wakarimu wanaojaribu kuwasaidia wale wenye uwezo wa kujisaidia wenyewe. Lakini kitu cha kwanza nchi za magharibi ziache kuzidi kuharibu mambo kwa kulazimisha serikali za Afrika kubinafsisha uchumi wao, na kulazimisha kuingia katika masoko yasiyo na ushindani wenye haki.

MAKALA HII IMETAFSIRIWA KUTOKA KWENYE MAKALA ILIYOANDIKWA NA Nick Dearden ni Mkurugenzi wa taasisi ya Uingereza ya  Global Justice Now. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa  Jubilee Debt Campaign.
KWA KUSOMA MAKALA HALISI BONYEZA HAPA

Alhamisi, 18 Mei 2017

RC MAKONDA ATOA MAELEKEZO 17 KWA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI NA UJENZI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 akizungumza Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam

Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakimsikiliza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 wakati wa kikao cha kuimarisha utendaji
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda wakati wa kikao cha Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Leo Mei 18, 2017.
Baadhi ya Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakifuatilia kikao cha kazi kilichoongozwa na Rc Makonda

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda  Mei 18, 2017 alizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, na alitoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.

1.Watendaji wa sekta ya Ardhi Na Ujenzi kushughulikia migogoro ya ardhi na ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu.

2.Watendaji wa sekta ya Ardhi na Ujenzi wameagizwa kutoa vibali vya ujenzi ndani ya mwezi mmoja na zoezi hilo lianze mwezi wa sita mwaka huu 2017. Mwanzoni mwa mwezi wa saba kutazinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.

3.Wakuu wa Idara katika sekta ya Ardhi na Ujenzi kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu mipango ya idara kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana mahusiano na waandishi mbalimbali katika  vyombo vya habari.

4.Wakuu wa idara ya Ardhi na Ujenzi kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa hati, na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa hati za maeneo ya wazi kama wapo.

5.Wakuu wa Idara ya Ardhi na Ujenzi kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya umma kama kama vile Shule, Hospitali, na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba na kutoa mikakati wa upimaji.

6.Wakuu wa idara ya Ardhi na Ujenzi kuhakikisha ufanisi na bidii ya utendaji inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani mji ukipimwa vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya ardhi.

7.Kushughulikia changamoto za kisera unaofanya utaratibu wa upimaji na utoaji wa hati kuchelewa kukamilka.

8.Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa na utendaji imara unaoshabihiana na jambo la kisera.

9.Kila mtumishi kufanya kazi yake kwa uaminifu kwani dhamana aliyopewa ni kubwa na anapaswa kuitendea haki. Watumishi wote kusimamia na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho kimeingia mkataba Na wananchi katika kipindi cha miaka mitano.

10.Kila Mkuu wa Idara kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015-2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake sambamba na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma na kuielewa vyema ilani hiyo.

11.Kufatilia na kufahamu upandaji wa madaraja Na stahiki zao kwani ni haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja na kwenda likizo.

12.Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika.

13. Kuwa na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa kazi.

14.Kujitokeza ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha na utoaji wa hati za ardhi kinyume na sheria. Na endapo wasipojitokeza na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.

15.Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze kuelewa. Sambamba na kutoogopa maazimio kama wanatenda kazi kwa mujibu wa sheria pasipo kupendelea.

16.Wakuu wa Idara kila mwisho wa wiki kutoa taarifa kwa Wakurugenzi inayoonyesha idadi ya migogoro na jinsi ilivyotatuliwa.

17.Katika kupunguza changamoto ya kuwafikia wananchi kwa Wakati RC Makonda amesema atatoa pikipiki 5 katika sekta ya Ardhi kwa kila Manispaa.