HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 12 Aprili 2017

AFANDE KUMAPAYI ASIMAMISHWA KAZI KWA UCHUNGUZI


Afande akitoa adhabu

Nywele zilizokatwa

Kazi moja tu


Matrafiki wa kike wa kituo kimoja huko Naijeria wamekutana na kasheshe kubwa baada ya kiongozi wao mmoja Andrew Kumapayi, ambaye ni kamanda wa mkoa Federal Road Safety Corp (FRSC), kikosi cha trafiki cha  Rivers State Kusini, kuwakata nywele askari wa kike wa kikosi hicho  waliokuwa na nywele ndefu wakati wa paredi ya kukagua usafi. Kiongozi huyo ambaye sasa nae kasimamishwa kazi na wakubwa zake alipigwa picha akiwakata rasta askari hao wa kike, kama adhabu ya kuwa na nywele ndefu. Jambo hili la kudhalilisha akina mama limeleta mtafaruku mkubwa huko. Sheria za jeshi hilo zinaruhusu akina mama kuwa nywele ndefu mradi tu ziwe zinaweza kufichwa kwenye kofia, sheria hazijaongoza nywele ziwe na urefu gani. Picha za mkasa huo awali zilitupiwa na jeshi hilo kwenye ukurasa wake wa facebook, lakini sheshe lilipoanza zikaondolewa, bahati mbaya wananchi walikwisha jisambazia. Maelezo ya picha yalikuwa yanasema Afande Kumapayi alikuwa anakagua kucha na nywele siku hiyo. Maafisa wengine waliokuweko kwenye tukio hilo nao wanachunguzwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni