HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Alhamisi, 6 Aprili 2017

BAADA YA MASHOGA KUPATA KIPIGO ALFAJIRI JUMAPILI


Baada ya mashoga wawili Jasper Vernes-Sewratan mwenye umri wa miaka 35 na Ronnie Sewratan-Vernes wa miaka 31 kupata kipigo mtaani huko Netherland siku ya Jumapili, wanaume wa Kiholanzi wa kila kada wameanzisha kampeni ya kupiga picha huku wameshikana mikono na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii kama njia ya kupinga kitendo hicho. Mashoga hao walidai kuwa walikula mkong’oto huo alfajiri ya Jumapili kutoka kwa kundi la watu. Habari hiyo ilishika nafasi katika vipindi mbalimbali vya TV. Mwanasheria wa jamaa wanaodaiwa kuwakong’ota mashoga hao alijitokeza na kudai kuwa mashoga hao ndio walioanzisha hizo ngumi. Kuna mashoga wengine nao kutoka miji ya Amsterdam na Eindhoven nao wamelalamika kuwa walikong’otwa kwa kukutwa wameshikana mikono wakati wanatembea barabarani. Uholanzi ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu ndoa za jinsia moja kisheria mwaka 2001.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni