HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumamosi, 8 Aprili 2017

KABURI LA YESU KRISTU HATIMAE LAFANYIWA UKARABATI


Kaburi likikarabatiwa

Sehemu ya kuabudia
Baada ya miezi tisa ya matengenezo, hatimae watu wameruhusiwa tena kufika na kufanya sala zao katika eneo ambalo linaaminika ndipo alipo zikwa Yesu Kristo. eneo hilo la kaburi liko katikati ya sehemu ya Wakristo katika mji wa Jerusalem ya zamani, lililazimika kufanyiwa ukarabati kutokana na kuchakaa kwa umri. Kaburi hili lilijengewa kwa mara ya kwanza katika karne ya 4, na kutambulishwa kuwa ndipo mahali ulipopumzishwa mwili wa Yesu Kristu baada ya kusulubiwa. Mradi huu ulisimamiwa na na World Monument Fund, wakati Antonia Moropoulou wa National Technical University ya Athens aliongoza jopo la wataalamu walioifanya kazi hiyo ya kulikarabati kaburi hilo. Kaburi hili lilikuwa likikarabatiwa usiku tu ili kuruhusu watu wengi ambao hufika kusali hapo waendelee na ibada zao wakati wa mchana. Mwezi Oktoba mwaka jana mafundi walilifungua kwa mara ya kwanza kaburi hilo lililofunikwa na mfuniko wa jiwe  miaka 500 iliyopita, na hapo ndipo wanasayansi nao waliokuwepo waliweza kuona na kupima jiwe halisi ambalo linasemekana ndimo ulimowekwa mwili wa Yesu Kristo baada ya kifo msalabani. Madhebu sita hushirikiana kuabudu katika sehemu hii yakiwemo; Franciscan (Wakatoliki), WaCoptic, Makanisa ya KiOrthodox ya Ethiopian, Syrian, Armenian, na Greek. Kutokana na kumalizika kwa kazi hii muda mfupi kabla ya Pasaka inategemewa maelfu ya Wakristu kutoka sehemu mbalimbali duniani watafika kuja kuabudu hapo mwaka huu. Bei ya ukarabati wa sehemu hii ulifikia  $3.72 milioni, iliyopatikana kutoka kwa michango ya watu binafsi na WFM trustee Mica Ertegun iliyotoa  $1.3 milioni kuunga mkono kazi hiyo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni