HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 18 Aprili 2017

KOREA KASKAZINI YAONYA KUHUSU UWEZEKANO WA VITA

BALOZI wa Korea kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa, ameionya Marekani iache mchezo wake wa kuitishia vita nchi yake kila mara na ameonya kuwa kuna uwezekano wa vita ya kinyuklia hali isipobadilika. Balozi huyo Kim In Ryong, siku ya Jumatatu alitoa maneno makali akielezea uwezekano wa kuitandika Marekani kwa silaha za nyuklia. Balozi huyo alilaani kuongezeka kwa majeshi ya Marekani jirani na Rasi ya Korea, na pia akalaani kitendo cha Marekani kuipiga mabomu Syria. Alisema Marekani imetengeneza mazingira ya hatari na vita inaweza kuanza wakati wowote na kuleta madhara makubwa duniani. Balozi huyo alisema Marekani inaharibu amani duniani kwa kutumia mbinu za kijambazi katika kuingilia uhuru wa mataifa mengine. Balozi aliwaambia waandishi wa habari aliowaita kuwa Marekani ikidondosha kombora nchini mwake nao watajibu mapigo kwa kudondosha kombora Marekani.  Msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema shirika hilo lina wasiwasi mwingi kuhusu hali ilivyo katika kipindi hiki, na kushauri taratibu za kidiplomasia ziongezeke mara dufu. 
Silaha zilizoonyeshwa hadharani na Korea Kaskazini hivi karibuni


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni