HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 12 Aprili 2017

MAANDAMANO YA KUTAKA ZUMA ANG'OKE YAPAMBA MOTO AFRIKA YA KUSINI

MAELFU ya waandamanaji wamejikusanya katika jiji la Pretoria Afrika ya Kusini wakishinikiza Rais Jacob Zuma aachie madaraka. Maandamano hayo yamefanyika kwa kushirikiana kwa vyama vya upinzani vya nchini humo, vikifuatiwa na maandamano yaliyofanyika nchi nzima wiki iliyopita. Hatua ya Rais Zuma kumfukuza kazi aliyekuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Pravin Gordhan kumekoleza moto hasira za wananchi juu ya tuhuma za rushwa serikalini, ukosefu wa ajira, na mdororo wa uchumi. Maandamano hayo yameongozwa na chama cha mlengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters (EFF) party, kikiambatana na Democratic Alliance (DA) na vyama vingine vidogo vya upinzani. Kwa mara ya kwanza kumeonekana upinzani ukishirikiana kufanya jambo kama hilo pamoja. Maandamano ya wiki iliyopita yalihamasishwa na vyama vya visivyo vya kisiasa na vikundi vya dini, kwa sasa vyama saba vimeungana kutaka kumng’oa Zuma
Chama tawala cha ANC kimekuwa kikijaribu kuziba ufa na hata kuonyesha kuwa kitamuunga mkono Zuma katika kikao cha Bunge wiki ijayo kitakachopiga kura ya kutokuwa na imani na Zuma. Kupiga kura huko kumechelewa baada ya kuingia katika mgogoro kuhusu aina ya upigaji kura, kuwa wa wazi au wa siri. Zuma, mwenye umri wa miaka 75 sasa anategemewa kumaliza muda wake wa kuongoza ANC mwezi December ili kukitayarisha chama chake  kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka 2019. Mpaka sasa inasemekana Zuma anapendelea mtalaka wake Nkosazana Dlamini-Zuma kurithi uongozi wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni