HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 4 Aprili 2017

MAHARAMIA WA KISOMALI WATEKA MELI NYINGINE


MAHARAMIA  wa Kisomali wameteka meli ya kibiashara ya India jirani kabisa na pwani ya Somalia. Hii ni meli ya pili kutekwa katika kipindi cha wiki mbili. Ni miaka kadhaa imepita kukiwa hakuna utekaji katika pwani ya Somalia. United Kingdom Maritime Trade Operations (UKMTO), taasisis ambayo huratibu meli za kibiashara katika Ghuba ya Aden ilisema kuwa ilipata taarifa ya kutekwa kwa meli iliyokuwa ikitoka Dubai kuelekea Bosasso, meli hiyo ilikuwa imetekwa jirani na kisiwa cha Socotra. Msemaji wa taasisi hiyo aliitaja meli hiyo kuwa inaitwa Al Kausar. Taarifa nyingine zilisema kuwa meli iliyotekwa ilikuwa na mabaharia 11 na ilikuwa ikipelkwa Eyl katika nchi ya Putland. Na watekaji walikuwa wanadai kulipwa fedha ambazo kiasi chake hakijatajwa.
Mwezi uliopita maharamia wa Kisomali waliteka meli ya mafuta lakini wakaaiachia baada ya mapigano na jeshi la majini la  Puntland. Inadaiwa Wasomali wamekasirishwa na wingi wa meli za uvuvi za kigeni zinazovua katika pwani yao

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni