HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 26 Aprili 2017

SINEMA YA UKUTA WA TRUMP INAENDELEA


KATI ya ahadi moja kubwa iliyomfanya Trump achaguliwe kuwa rais wa USA ni kuwaahidi wapiga kura kuwa atajenga ukuta kwenye mpaka wa nchi yake na Mexico ambao utawazuia watu kutoka Mexico wasivuke kwenda Marekani. Tena akaahidi kuwa Mexico ndio itakayolipia ukuta huo. Wiki hii Rais huyo amekwepa kupeleka kwenye Bunge la nchi yake maombi ya fedha za kujengea ukuta huo. Wabunge wa chama cha Democrats walitangaza mapema kuwa akileta bajeti hiyo wao wataipinga. , baadhi ya wabunge wa Republican pia walionekana hawatakubaliana na bajeti hiyo kwani italazimika waidhinishe $21.6 bilioni, badala ya $12bilioni ambazo awali Rais huyo alisema ndio zitahitajika kujenga ukuta wa Mexico. Mshauri wa Rais Kellyanne Conway, alitangaza rasmi kuahirisha ombi hilo la fedha hizo. Kama kawaida yake rais Trump alituma ujumbe kupitia Twitter kuwa ukuta huo iko siku utajengwa tu.  Kwenye ukurasa wake wa Twitter Trump aliandika  "Don't let the fake media tell you that I have changed my position on the WALL. It will get built and help stop drugs, human trafficking etc.". Hizo ndizo mbinu za wanasiasa dunia nzima

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni