HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 26 Aprili 2017

TIMU ZA NEWCASTLE NA WEST HAM ZAPELELEZWA KWA SKENDO YA UFISADI


Her Majesty's Revenue and Customs (HMRC), kitengo ch ukusanyaji wa kodi huko Uingereza, kimetumia zaidi ya wafanyakazi wake 180 kuchunguza ufisadi katika tasnia ya mpira wa miguu nchini humo. Na watu kadhaa wametiwa nguvuni.  Katika uchunguzi wao ofisi kadhaa zimepekuliwa,na nyaraka nyingi  zikiwemo taarifa za mapato na matumizi, simu za mkoni , kompyuta, mafaili na taarifa mbalimbali za watuhumiwa pia zimekamatwa kwa uchunguzi. Maafisa kutoka Ufaransa wanasaidiana na maafisa hawa wa Uingereza kukamata wahalifu. Ofisi za timu maarufu za Newcastle United na West Ham United pia zilipekuliwa  katika uchunguzi huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni