HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatatu, 3 Aprili 2017

UNAKUMBUKA VIDEO YA MSICHANA WA KAZI AKIANGUKA TOKA GHOROFANI UARABUNI? PATA KILICHOENDELEA


Siku chache zilizopita , video ya msichana wa kazi akianguka kutoka ghorofani ilikuwa inazunguka katika mitandao ya kijamii haswa Whatsapp. Hatimae hadithi nzima sasa imejulikana. Video hiyo inayotisha ilipigwa na mama mmoja nchini Kuwait. Sasa mama huyo amefikishwa mahakamani. Katika video hiyo msichana wa kazi alikuwa kajishikilia kwa mkono mmoja kwenye pembe ya dirisha akiomba msaada maana alikuwa hatarini kudondoka kutoka ghorofani. Wizara ya Sheria ya Kuwait imesema kuwa mwanamke wa Kikuwait aliyerekodi video hiyo ya sekunde 12, amekamatwa na atashtakiwa kwa makosa mawili,
i.               kumpiga picha mtu bila ridhaa yake
ii.              kuisambaza video hiyo bila ruksa ya mhusika
Katika video hiyo sauti ya mama wa Kikuwait inasikika ikisema ‘Rudi we mwenda wazimu’ wakati binti aliyekuwa kwenye hatari ya kuanguka akilia na kuomba, ‘Nishike nishike’. Baada ya hapo alishindwa kuendelea kujishikilia na kudondoka kutoka ghorofani. Alipofikishwa hospitali iligundulika kuwa amevunjika mkono, lakini hakuwa na madhara ya kutishia uhai wake. Mkasa huu ulitokea 30 March 2017, katika wilaya ya Sabah al-Salem ya jiji la Kuwait City. Chama cha Haki za binadamu cha Kuwait kimetoa tamko kulaani kitendo hicho, chama hicho kilisisitiza serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo. 
Wakati wa upelelezi, mama huyo wa Kikuwait alipoulizwa ilikuwaje akachukua video ya kitendo kile cha kutisha? Yeye alijitetea kuwa alikuwa jikoni akipiga picha chakula alichokuwa amekitengeneza, ndipo binti yake alipomtaarifu kuwa msichana wao wa kazi alikuwa katoka nje kupitia dirishani, alipoingia katika chumba hicho video iliendelea kuchukua matukio. Alipoulizwa kwanini hakumsaidia yule binti, akajibu msichana huyo wa kazi ni mzito aliogopa angemsaidia na yeye angeanguka. Alipoambiwa kuwa inasemekana kuwa binti huyo alikuwa akiteswa sana hivyo alikuwa akijaribu kutoroka, mwajiri alijibu kuwa msichana mwenyewe alikuwa ameanza kazi siku chache tu zilizokuwa zimepita. Binti huyo ni raia wa Ethiopia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni