HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 4 Aprili 2017

URUSI YATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO

Mtu aliyesababisha vifo vya watu 11 kwenye mlipuko wa treni katika jiji la St Petersburg inadaiwa kuwa alikuwa ni mtu kutoka Kyrgyzstan ambaye alichukua uraia wa Urusi. Watu zaidi ya 45 walijeruhiwa katika tukio hilo na serikali ya Urusi imetangaza siku 3 za maombolezo. Bado kuna utata kuhusu uhai wa mtu huyo ambaye anasemekana alikuwa na umri wa miaka 23. Kuna habari kuwa alijitoa mhanga katika mlipuko huo ndani ya treni. Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mauaji hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni