HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumamosi, 15 Aprili 2017

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAEL EHUD BARAK ATEMBELEA SERENGETI NA NGORONGORO

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani wa Israel,Ehud Barak walipokutana katika eneo la Olduvai Gorge katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Bwana Ehud Barak  alikuwa njiani kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (katikati) ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete.

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Barak (kushoto) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani baada ya kukutana katika eneo la Makumbusho ya kale la Olduvai Gorge ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro (kushoto) ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.

Mhandisi Ramo Makani akimueleza jambo Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Barak.
Naibu Waziri wa Malisili na Utalii (katikati), akimongoza Ehud Barak (kushoto) kutembelea eneo la Olduvai Gorge .kulia ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Waziri Mkuu wa zamani wa  Israel Ehud Barak akitia saini katika kitabu cha wageni huku Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani akishuhudia mara baada ya kufika eneo la Olduvai Gorge akiwa njiani kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushudia uhamaji wa makundi makubwa ya  Nyumbu.
Mhandisi Ramo Makani akimueleza jambo Ehud Barak.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akieleza mambo ambayo aliongea na Waziri Mkuu wa Israel baada ya kukutana nae katika eneo la Olduvai Gorge.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwa katika picha ya pamoja na Watalii wa ndani baada ya kukutana nao katika eneo la Olduvai Gorge.

Habari na picha kwa hisani ya Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni