HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 26 Mei 2017

AFRIKA SIYO MASIKINI, AFRIKA INAIBIWA


MAKALA HII IMETAFSIRIWA KUTOKA KWENYE MAKALA ILIYOANDIKWA NA Nick Dearden ni Mkurugenzi wa taasisi ya Uingereza ya  Global Justice Now. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa  Jubilee Debt Campaign.

Afrika si masikini, lakini tunaweza kuwasaidia watu wake. Ni ujumbe rahisi unaorudiwa katika maelfu ya picha, habari katika magazeti, na wakati wa maombi ya michango ya kupeleka Afrika kila mwaka, kwa sababu hiyo jambo hilo hatimae linaanza kuchukua nafasi ya ukweli.

Tukisoma tena na tena ujumbe huo , tunazidi kuhakiki ukweli kuhusu hadithi ambazo tumekuwa tukizisikia kuhusu Afrika maisha yetu yote. Picha tuliyonayo ya Afrika inazidi kuwa ya kweli.

Hebu tujaribu kupata ujumbe tofauti.

Afrika ni tajiri lakini tunaiibia mali yake. Ujumbe unakuwa kama uwongo, lakini ujumbe huu ndio mwelekeo wa ripoti  (pdf) iliyotayarishwa na vikundi vya kiharakati mbalimbali iliyotolewa hivi karibuni. Ripoti hii ikiwa imejikita na takwimu inaonyesha kuwa nchi za Afrika kusini mwa Sahara zina deni la zaidi ya $41bn.   
Ni kweli kuna fedha za zinazoingia katika nchi hizi kutoka nchi za nje, kiasi cha  $161bn  kwa mwaka, lakini fedha hizi ni mikopo, fedha zinazotumwa na wananchi wa nchi hizi wanaofanya kazi nchi za nje, na misaada mbalimbali. Lakini wakati huohuo kuna kuna kiasi cha $203bn kinahamishwa kutoka nchi hizi, kati ya hizo $68bn zikiwa ni pesa kutokana na kukwepa kodi. Makampuni ya kimataifa ‘huiba’ hizi fedha 'kihalali',  kwa kudai kuwa wao hupata faida yao kutokana na kuzihifadhi katika nchi zenye unafuu wa kodi na sio Afrika. Taratibu hizi zinazoitwa "illicit financial flows" huchukua kiasi cha asilimia 6.1 ya pato  (GDP) lote la bara la Afrika, au ni sawa na mara tatu ya misaada ambayo Afrika hupewa. Baada ya hapo kuna $30bn ambayo makampuni ya kimataifa huhamisha kutoka Afrika kwenda kwao kama faida ambazo kampuni hizi hupata kutokana na shughuli zinazofanya Afrika. Jiji la London limefurika na faida zilizokamuliwa kutoka kwenye ardhi na nguvukazi za Afrika. 
Kuna njia nyingi ambazo hutumika kukamua utajiri wa Afrika. Ukataji miti usio halali, uvuvi haramu, na biashara haramu ya wanyamapori unakamua $29bn  kwa mwaka. Hasara nyingine ya $36bn huingizwa kila mwaka kutokana na uharibifu unaoleta mabadiliko hasi ya tabianchi. Pamoja na kuwa uharibifu mkubwa mazingira ulioko Ulaya haufanywi na Waafrika lakini bila shaka matokeo ya mabadiliko ya tabianchi yatawaathiri Waafrika zaidi. Na hakuna mpango wowote wa kufidia hali hiyo.
Kiukweli hata kama kungekuwa na malipo yanayopelekwa Afrika, utafiti unaonyesha kuwa mtizamo uliopo kuwa misaada inayoingia Afrika inawanuafaisha watu wa bara hilo, si kweli kwani mikopo inayochukuliwa na serikali na taasisi binafsi, ambayo ni zaidi ya  $50bn huishia kuwa madeni yasiyolipika. Nchi ya Ghana inapoteza asilimia 30 ya mapato ya serikali kulipia madeni, madeni yaliyotokana na miradi ambayo haikutekelezeka, ambayo ilikuwa na riba kubwa kupindukia. Kwa mfano Msumbiji iliwahi kuchukua mkopo wa kujengwa mtambo wa kuyeyusha alumini, kwa sasa mtambo huo unaigharimu serikali ya Msumbiji  £21 kwa kila  £1 ambayo serikali ya Msumbiji inapata. Msaada wa Uingereza (British aid), unaotumika kuanzisha shule na hospitali za kulipia za binafsi, zinasababisha kupunguza kwa kasi ya kutengeza hospitali na shule za umma nzuri, jambo ambalo limeanza kusababisha shule za namna hiyo kuanza kufungwa Uganda na Kenya.  Lakini katika mazingira haya haya kuna Waafrika ambao wanatajirika sana. Takwimu zinaonyesha kwa sasa kuna Waafrika kiasi cha 165,000 ambao ni matajiri sana, kwa pamoja wanautajiri wa $860bn. Lakini kwa jinsi uchumi unavyofanya kazi matajiri hawa fedha zao hawaziweki Afrika, wameziweka katika nchi zile ziitwazo ‘tax havens’. 2014 kulikuwa na makisikio kuwa Waafrika hawa matajiri wana kiasi cha $500bn wameziweka katika benki za ‘tax havens’.  Watu wa Afrika wanaibiwa utajiri wao na aina ya uchumi ambao unawawezesha watu wachache kutajirika na hatimae kuhamisha uchumi huo kutoka Afrika.

Sasa nini kifanyike?  Nchi za magharibi hujinasibu kuwa ni wakarimu wanaojaribu kuwasaidia wale wenye uwezo wa kujisaidia wenyewe. Lakini kitu cha kwanza nchi za magharibi ziache kuzidi kuharibu mambo kwa kulazimisha serikali za Afrika kubinafsisha uchumi wao, na kulazimisha kuingia katika masoko yasiyo na ushindani wenye haki.

MAKALA HII IMETAFSIRIWA KUTOKA KWENYE MAKALA ILIYOANDIKWA NA Nick Dearden ni Mkurugenzi wa taasisi ya Uingereza ya  Global Justice Now. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa  Jubilee Debt Campaign.
KWA KUSOMA MAKALA HALISI BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni