HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 10 Mei 2017

BINTI ALIYETEKWA NA BOKO HARAM AGOMA KURUDI KWA WAZAZI WAKE, NI BAADA YA KUPATA MUME MPIGANAJI WA BOKO HARAM


Wasichana walioachiwa wakiongea na Rais wao siku ya Jumapili baada ya kuachiwa huru
Mmoja kati ya mabinti waliotekwa na Boko Haram, amegoma kurudi kwa wazazi wake na kuamua kuendelea kuishi na mumewe mpiganaji wa Boko Haram. Jumapili iliyopita kundi la wasichana kati ya wale waliotekwa na Boko Haram  miaka mitatu iliyopita lilikabidhiwa kwa serikali ikiwa ni katika makubaliano ambapo serikali ya Nigeria nayo iliwaachia wafungwa kadhaa wa Boko Haram. Mpaka sasa Boko Haram bado inawashikilia wasichana 100 kati ya 276 ambao iliwateka.  Msemaji wa Rais wa Nigeria alisema, “Ilikuwa waachiliwe wasichana 83 lakini mmoja alisema hana tatizo maana amekwisha pata mume”. Inasemekana kundi hilo la Boko Haram limeteka maelfu ya watu katika jimbo ambalo wapiganaji hao wanalizunguka. Inaaminika kuwa kati ya wasichana waliotekwa, wengine waliozeshwa kwa wapiganaji hao na wamezaa nao watoto. 
Kazi ambayo bado haijakamilika ni kuwarudisha mabinti hawa walioachiwa kwa wazazi wao, serikali ilisambaza majina yao kwenye mitandao ya kijamii lakini inaeleweka wazi si wazazi wote wanatumia huduma hiyo. Aisha Yesufu mratibu wa kampeni ya
#BringBackOurGirls, alisema wanajitahidi kuhakikisha wasichana wanaunganika na wazazi wao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni