HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 10 Mei 2017

MAREKANI YAZUIA MSAADA WA DOLA MILIONI 21, KWA WIZARA YA AFYA KENYA


SERIKALI ya Marekani imesimamisha msaada wa dola milioni 21 uliokuwa uende kwenye Wizara ya afya ya Kenya, kutokana na tuhuma za rushwa katika Wizara hiyo. Jambo hilo litaongeza mzigo kwa serikali iliyopo madarakani katika uchaguzi mkuu unaokuja karibuni. Marekani huingiza zaidi ya dola 650 milioni kila mwaka kwa ajili ya Wizara ya Afya ya Kenya. Taarifa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini humo ilisema, “Tumechukua hatua hii kutokana na ripoti za rushwa na taratibu hafifu za uwekaji wa mahesabu ya fedha katika Wizara hii, na tunajaribu kufanya kazi pamoja na Wizara hii kuboresha uwekaji wa Mahesabu”
Taarifa hii inaongeza uzito wa tuhuma kadhaa zinazoiandama serikali ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye yuko mbioni kuomba kura ili atawale kwa kipindi cha pili na cha mwisho cha miaka mitano, katika uchaguzi mkuu hapo tarehe 8 Agosti 2017. Katika kile kilichopewa jina la ‘Afya House scandal’,  mahesabu ya Wizara hiyo yaliwekwa hadharani na vyombo vya habari vya nchi hiyo na kuonyesha kuwa Wizara hiyo ilikuwa haina maelezo kuhusu matumizi ya shilingi bilioni 5 za Kenya (dola 49 milioni). Na mahesabu hayo pia yalionyesha kuwa fedha zilizopangwa kwa jili ya kutoa huduma ya uzazi bure pia hazikutumika kwa kazi hiyo.  Mwaka jana, kiongozi wa taasisi inayoshughulika na rushwa nchini humo alisema theluthi ya bajeti ya serikali inapotea kutokana na rushwa kila mwaka, fedha kiasi cha dola bilioni 6. Serikali ya Kenya inapinga kiasi hicho na kudai kinakuwa kikubwa kutokana na matatizo ya kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuweka mahesabu tu na si rushwa. Mwezi Oktoba mwaka jana Rais Kenyatta aliwashangaza Wakenya pale aliposema anashindwa kushughulikia vizuri rushwa kwani mikono yake ilikuwa imefungwa na kulaumu mahakama na taasisi nyingine kwa kutofanya kazi zao vizuri.
Madaktari na manesi wa Kenya wamekuwa wakilalamika kuwa hospitali hukosa vifaa vya msinghi kuanzia dawa na hata gloves kutokana na rushwa. Kwa muda mrefu madaktari wa nchi hiyo walikuwa katika mgomo wakidai masilahi zaidi kutokana na kazi yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni