HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 16 Mei 2017

NILIPOKARIBISHWA KAHAWA KWENYE SHOWROOM YA MAGARI YA FORD


Leo nimepata bahati kubwa sana nimekaribishwa katika duka la kuuza magari aina ya Ford lililoko Mtaa wa Maktaba Dar es Salaam, nimekaribishwa kikombe cha kahawa ya maziwa na kuweza kuangalia magari mbalimbali yaliyokuweko. Duka hili mali ya CMC Automobile Ltd. Pengine nikisema duka nakuwa sieleweki sawasaw labda niseme ‘Showroom  ya magari’. Hakika magari ya Ford ni mazuri sana. Lakini labda nirudi nyuma kidogo, nianze na historia ya magari haya aina ya Ford.  Kampuni ya magari ya Ford ilianza mwaka 1903. Kampuni ilizaliwa kutokana na juhudi binafsi za Henry Ford. Henry Ford aliunda gari lake la kwanza nyumbani kwake Detroit mwaka 1896, akaliita quadricycle. Baada ya hapo akiwa na wenzie wakatengeneza kampuni ikaitwa Detroit Motor Company mwaka 1899, lakini haikuchukua muda wafadhili wakaondoka na  mwaka 1901 ikafa na kampuni mpya iliyoitwa Henry Ford Company ikaanza nayo haikuchukua muda ikafa. Ford akabaki na haki ya jina na dola 900 tu mkononi. Akaanza kuwatafuta marafiki wenye pesa na kuwauzia wazo la kuanzisha kampuni ya kutengeneza magari, ikumbukwe wakati huo kulikuwa hakuna magari, na wazo hilo lilionekana kama la mwendawazimu. Katika hangaika yake hatimae tarehe 16 June 1903 kampuni ya Ford Motor Company ilisajiliwa.  Ford siku hizi iko dunia nzima, lakini hili halikutokea kwa siku moja ni kazi ambayo imechukua zaidi ya miaka 100. Gari za kwanza maarufu za Forf zilikuwa zile zilizojulikana kama Model T, na ndizo zilianza kuiletea faida kampuni hii ambayo imeshatengeneza magari ya aina mbalimbali. Mwaka 1945 mtoto wa kwanza wa Henry Ford aliichukua kampuni na kuiendeleza na kuanzia hapo matokeo yake ndio haya niliyoayaona leo. Kampuni ina magari madhubuti yaliyofanyiwa utafiti wa miaka mingi sana. Kati ya gari ambazo zipo katika show room ya Dar es Salaam nilizochungulia ndani na kuzipenda ni hizi hapa chini, japo zipo aina nyingi na rangi mbalimbali. 
FORD KUGA


 FORD RANGER


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni