HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 10 Mei 2017

TRUMP AMFUTA KAZI BOSI WA FBI


James Comey
Donald Trump kamfukuza kazi Mkurugenzi wa FBI James Comey, taarifa kutoka White House zinasema kuwa Mkurugenzi huyu amefukuzwa kutokana na ushauri wa Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions.
Katika barua ya kufukuzwa kazi ambayo James Comey ameandikiwa na Rais wake, moja ya sababu ambazo zimefanya afukuzwe ilikuwa ni... "not able to effectively lead"  na kuwa FBI inahitaji uongozi mpya ili kuaminika zaidi. Itakumbukwa kuwa Mkurugenzi huyu pia alilalamikiwa na Democrats kuwa alitoa taarifa zilizosababisha Mama Clinton kunyimwa kura. James Comey amekiri kuwa taarifa alizozitoa kuhusu emails za siri  hazikuwa sahihi.
Rais mpya wa Korea Kusini na mkewe
Jambo jingine jipya ni kuwa Korea Kusini imepata Rais mpya anaitwa Moon Jae-in, na tayari amekwisha sema angependelea kuwa na mazungumzo na kiongozi wa Korea kaskazini, jambo ambalo ni wazi halitaifurahisha Marekani. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni