HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumatano, 17 Mei 2017

UBALOZI WA MAREKANI WASAINI MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA NA ZIFF

U.S. Charg├Ęd’Affaires Virginia Blaser and ZIFF Director Fabrizio Colombo
LEO tarehe 17 May 2017, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetiliana saini ushirikiano na tamasha l Zanzibar International Film Festival (ZIFF), ambapo kwa ushirikiano huu, muongozaji wa filamu Judd Ehrlich na mtaalamu wa mambo ya filamu Debra Zimmerman wote kutoka Marekani watakuwa Tanzania kati ya tarehe 9-16 Julai 2017. Kaimu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser alitia saini kwa niaba ya Ubalozi na Mkurugenzi wa tamasha la ZIFF Fabrizio Colombo aliweka saini makubaliano hayo kwa niaba ya ZIFF.Judd Ehrlich ndiye aliyeongoza filamu ya Keepers of the Game, filamu inayofuatilia maisha ya timu ya wasichanwenyeji halisi wa Marekani waliokuwa wameweka nia ya kushinda kikombe katika mchezo wa lacrosse, mchezo ambao kwa asili umekuwa unachezwa na wavulana na wanaume tu.
Judd Ehrlich
Debra Zimmerman ni mtaalamu wa filamu na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayoitwa Women Make Movies, taasisi iliyojikita katika kufungua na kuongeza fursa za watengeneza filamu wanawake.
Debra Zimmerman
Kwa ushirikiano huu wa Ubalozi na ZIFF, Zimmerman na Ehrlich watashirikiana na watengeneza filamu kutoka Zanzibar katika tamasha la ZIFF ambalo linatimiza miaka 20. Wataalamu hawa wataendesha semina na warsha mbalimbali kuhusu utengenezaji wa filamu zinazohusu maisha halisi, masoko ya filamu na usambazaji wa filamu. Na kutakuweko warsha maalumu kwa wanawake walioko katika tasnia ya filamu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni