HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 2 Mei 2017

VURUGU ZAMAFANYA ZUMA ASHINDWE KUHUTUBIA MKUTANO WA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI


Vurugu kati ya wanaomuunga mkono Rais Jacob Zuma na wale wanaompinga zimesababisha  Rais huyo kushindwa kuhutubia mkutano wa Siku ya Wafanyakazi duniani, na kulazimika kukimbizwa kutoka jukwaani kwa usalama wake. Chama kikuu cha wafanyakazi cha Afrika ya Kusini (COSATU) kilimtaka Jacob Zuma ajiuzuru toka mwezi uliopita baada ya kumfuta kazi waziri wake wa Fedha.  Zuma na wanaomuunga mkono wanasisitiza kuwa lazima amalize kipindi chake kinachoishia mwaka 2019. Hali ilikuwa mbaya na ililazimika Rais huyo akimbizwe kutoka kwenye uwanja wa mkutano huko Bloemfontein city, tukio likionekana mubashara kwenye luninga. Rais Zuma aliamua kuja kuhudhuria mkutano huo licha ya chama shirika cha COSATU, Congress of South African Trade Unions kupinga uwepo wake. COSATU kina uhusiano mzuri na chama cha Zuma cha African National Congress (ANC).


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni