HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 2 Juni 2017

MWANAMKE MKENYA AHUKUMIWA KIFO MALAYSIA


MWANAMKE  mkenya wa miaka 40 amehukumia adhabu ya kifo na Mahakama Kuu ya Malaysia kwa kukutwa na hatia aya kusafirisha madawa ya kulevya. Mama huyu Rose Achieng Ojala alikuwa kaficha madawa mengine sehemu zake za siri na akiwa amememza kete 68, alikamatwa  uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur akitokea Addis Ababa siku ya tarehe 30 Novemba 2013.  Wasiwasi wake alipofika uwanja wa ndege huo ndio uliowafanya askari kumshuku na hatimae kukutwa na janga hilo, mwenyewe alisema rafiki yake wa kiume ndie aliyembebesha mzigo huo.
Hukumu ya mama huyu ilipitishwa na  Jaji Wong Teck Meng siku ya Jumapili. Alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwa madawa aliyokuwa ameficha sehemu za siri na kahukumiwa kifo kwa kete alizokutwa nazo. Kabla kesi haijaanza mama huyo mwenye watoto watatu alizimia na alilazimika kubebwa kuingizwa mahakamani kwa kutumia kiti chenye magurudumu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni