HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Ijumaa, 2 Juni 2017

RIAS TRUMP AJITOA MAKUBALIANO YA KUTUNZA HALI YA HEWA
Kumekuwa na fadhaa dunia nzima baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuamua kuitoa nchi yake katika makubaliano ya '2015 Paris climate agreement', makubaliano haya ambayo yalitiwa saini na Rais Barack Obama yalikuwa yanazitaka nchi zilizotia saini zaidi ya 195 kuhakikisha kuwa joto la dunia halizidi nyuzijoto sentigred 2 kufikia mwisho wa karne hii, na ikiwezekana hata lisizidi nyuzi1.5. Uamuzi huu unatokana na utafiti unaoonyesha kuwa matumizi mabaya ya mazingira yanaongeza kwa kasi joto la dunia na hivyo kusababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewana kuleta mafuriko, ukame, baridi kali na joto kali. Kati ya viongozi walioonyesha kukerwa na uamuzi huo wa Marikani ni Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye kwa lugha ya kidiplomasia ameita kitendo hicho ni cha kusikitisha sana, wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema hata mhukumu Trump. Katika hotuba yake ya kujitoa Rais Trump amedai kuwa makubaliano hayo ya Paris yalikuwa yakitesa Marekani na yeye alichaguliwa na watu wa Marekani na si Paris. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na hali ya hewa, UN World Meteorological Organisation  lilisema kujitoa kwa Marekani kuneweza kusababisha joto likapanda kwa nyuzi 3 kufikia mwisho wa karne hii na hapo, ulimwengu utakuwa umejiingiza kwenye tatizo lisiloweza kurekibishwa tena.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni