HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Jumanne, 29 Agosti 2017

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA NDG: RODRICK MPOGORO AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA MAKATIBU WA UVCCM MIKOA YA TANZANIA BARA NA VISIWANI

Naibu katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Rodrick Mpogoro akifungua mafunzo elekezi kwa Makatibu wa Umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati  kuu ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana na mjumbe wa kamati kuu  ya Chama Cha Mapinduzi Ndg Sadifa Juma khamisi akizungumza katika mafunzo  elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam
 Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika mafunzo elekezi kwa Makatibu wa Umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam


Washiriki wa mafunzo elekezi wakifuatilia mafunzo
Mshiriki Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa K ilimanjaro, Ndg Abdulrahim Hamid akiuliza swali wakati wa mafunzo  elekezi kwa makatibu wa Umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

KINANA AMWANDALIA BALOZI WA CHINA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KUMUAGA


 Katibu  Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Agosti 27, 2017. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Naibu Spika Tulia Akson, Mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Mawaziri Kadhaa, Makatibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Makatibu wa Jumuia za Chama. Picha zote na Bashir Nkoromo.
 Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kupokea zawadi maluum, ambayo Kinana alimzawadia wakati wa chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga.

MAGAZETI YA LEO 29 AGOSTI 2017
Jumamosi, 26 Agosti 2017

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI APITA FERRY WAKATI AKIELEKEA KIGAMBONI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akichukua Tiketi zake pamoja na chenchi mara baada ya kulipia huduma ya Kivuko wakati akielekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana pamoja na kuzungumza na abiria mbalimbali wakati akisubiri kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 26 AGOSTI 2017
Ijumaa, 25 Agosti 2017

ZAIDI YA SH BILIONI 200 KUWANUFAISHA VIJANA NCHINI

Waziri  wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kushoto) akiwasili katika taasisi ya Chuo cha Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) kuzindua mradi wa Vituo vya umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji zinazoleta tija  uliofadhiliwa na Benki ya Dunia,  kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NM-AIST Profesa David Mwakyusa na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo Profesa Karoli Njau .

Waziri wa Elimu, Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akipata  maelekezo juu ya utendaji wa Kituo hicho

Waziri  wa Elimu, Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizindua mradi wa Vituo vya Umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somalia Bella Bird.
Na Filbert Rweyemamu, Arusha
Benki ya Dunia imetoa Sh 200 Bilioni  ili kuwezesha miradi ya elimu na ujuzi kwa ajili ya kazi zinazoleta uzalishaji wenye tija pamoja na vituo viwili vya umahiri vya kikanda vitakavyofungua ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu elimu.

Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta za kilimo,utalii,ujenzi ,nishati na madini.


Alisema  kuwa miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na vituo vinne vya umahiri katika masuala ya utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pia ipo miwili iliyochini ya taasisi ya Chuo Kikuu ya Nelson Mandela pamoja na vituo vingine viwili vilivyopo katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine(Sua).


Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia, Bella Birds alisema kuwa uboreshwaji wa rasilimali watu kwa kuongeza ujuzi uliokosekana utasaidia taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa viwanda.


Bella alisema inakadiriwa kuwa vijana milioni 1 huitimu katika vyuo na kuingia katika soko la ajira kila mwaka hivyo anatarajia kuwa nafasi za ajira kwa vijana hao zitatengenezwa na sekta binafsi iwapo zitashirikiana vyema na serikali .


Makamu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Karoli Njau alisema kuwa mradi huo utasimamiwa kwa makini ili kuhakikisha kuwa malengo yanafikiwa hususan katika vituo vya umahiri pamoja na mradi wa ujuzi.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi  Tanzania (TPSF), Godfrey  Simbeye amesema kuwa kulikua na upungufu mkubwa wa watu wenye ujuzi nchini kutokukidhi mahitaji ya soko la ajira hivyo kulazimu waajiri kuajiri watu kutoka nje jambo linalogharimu fedha nyingi hivyo mradi huo utasaidia vijana 30,000 kupata ujuzi utakaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

MAGAZETI IJUMAA 25 AGOSTI, 2017
Alhamisi, 24 Agosti 2017

KINANA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI ZA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, LEO JIJINI DAR ES SALAAM


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akiwa katika mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, alipokutana nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akiwa na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, baada ya mazungumzo nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini. 
PICHA: BASHIR NKOROMO. KWA PICHA ZAIDI ZA KIKAO HICHO/>BOFYA HAPA

AFISA MTENDAJI MKUU WA STANDARD CHARTERED BANK-TANZANIA, ABADILISHANA UZOEFU WA KAZI NA WAFAYAKAZI WA AIRTEL LEO

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, (kushoto), akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao (Network), Bw. Emmanuel Luanda, Mkurugenzi wa IT, Bw. Frank Filman, na Mkurugenzi wa Masoko, Bw.Isack Nchunda. kampuni ya Airtel ilitembelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Charted bank ili kubadilishana uzoefu katika kuhudumia wateja wao.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, (kulia), na Afisa Mtendaji Mkuu, wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw. Anjay Rughani, wakizunhuzma kabla ya kuanza kwa semina hiyo.


Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati akimkaribisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, kutoa semina ya kuhamasisha (motivation), makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. kampuni ya Airtel ilitembelewa na Afisa Mtendaji Mkuu huyo kutoka Standard Charted Bank ili kubadilishana uzoefu katika kuhudumia wateja wao.Afisa Mtendaji Mkuu, wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw. Anjay Rughani, ambaye ni mmoja kati wa watanzania wachache wanaoshikilia nafasi hiyo ya juu kwenye taasisi za kimataifa, akizungumza wakati wa semina ya kuwahamasisha (motivation), wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airtel, makao makuu, jijini Dar es Salaam.
MAGAZETI YA LEO 24 AGOSTI 2017