HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Alhamisi, 10 Mei 2018

Airtel yaja na Fursa ya wekeza na Airtel Money Branch

  • Airtel yafungua milango kwa wawekezaji wa Airtel Shops branch nchini kote Tanzania

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Airtel money imedhamiria kuwakomboa Watanzania kwa kutoa ajira kwa kuanzisha ushirikiano wa uwekezaji na uendashaji wa maduka yake ya kisasa maarufu kama Airtel Money Branch.

Kwa wale ambao watapata fursa hiyo, kampuni ya Airtel itawawezesha kwa kiwapatia vifaa vyotebmuhimu ikiwemo kupiga chapa duka, floti kwenye akaunti ya Airtel Money pamoja na simu za kuendesha duka la Airtel Money kwa mafanikio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza ushirikiano wa uwekezaji huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda alisema kuwa Airtel ina nia ya dhati ya kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kujiajiri kupitia Airtel Money.

Airtel Fursa huwapa vijana fursa ya kuwakilisha ujuzi wao na wangependa kuufanikisha. Mpaka sasa, kuna mamia ya vijana ambao wameweza kufaidikia na kampeini ya Airtel Fursa na mpaka sasa wameweza kujiajiri na hivyo kubadilisha maisha yao. Kupitia Airtel Money branch tuna uhakika maelfu ya vijana wataweza kupata fursa ya kujiajiri na hivyo kubadilisha maisha yao.

Na ikiwa ni muendelezo wa Airtel Tanzania kuendelea kutoa fursa za kujiajiri kwa Watanzania, Airtel pia imeweza kufungua maduka ya huduma za simu mkononi nchini kote. Lengo ni kuendelea kufanya vijana wajiajiri lakini pia ni mpango kabambe wa kupeleka huduma karibu na wateja wake.

Maduka haya ya Airtel Money branch yana muonekano unaofanana na yako katika maeneo maalumu ambayo yatawawezesha maelfu ya wakazi kupata huduma kirahisi na kukidhi mahitaji yao kwa ufanisi zaidi

Maduka hayo yatatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kifedha, huduma za intaneti, kuongeza salio , kusajili namba na pia kuunganisha wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel.

Tunaamini hii ni njia pekee ya kuwafikia wateja wetu na kujua changamoto zao na kuzitatua kwa wakati na vilevile kuwaunganisha na huduma na bidhaa zetu za kipekee na kibunifu zinazosaidia kutatua changamoto zao za kila siku za kijamii na kiuchumi.


Kuanzishwa kwa maduka haya sehemu mbalimbali nchini kunadhihiriwha kwa vitengo dhamira ya Airtel kuendelea kuwekeza nchini na Afrika kwa ujumla.

 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akikata utepe wakati wa kuzindua moja kati ya maduka ya Airtel mkoani shinyanga ambapo jumla ya maduka 8 yatazinduliwa kwa lengo lakutoa ajira na kutoa huduma ya mawasiliano katika mkoa wa Shinyanga. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Airtel Tanzania,  Sunil Colaso akifuatiwa na Meneja wa Kanda ya kati wa Airtel , Bw Stephen Akyoo


Muonekano wa duka jipya la Airtel Money Branch lililopo Wilaya ya Chato mkoani Geita maalum kwa kutoa huduma za mawailiano za Mtandao wa Airtel.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni