HATUPIMI BANDO

HATUPIMI BANDO

Alhamisi, 10 Mei 2018

Airtel yaja na Fursa ya wekeza na Airtel Money Branch

  • Airtel yafungua milango kwa wawekezaji wa Airtel Shops branch nchini kote Tanzania

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Airtel money imedhamiria kuwakomboa Watanzania kwa kutoa ajira kwa kuanzisha ushirikiano wa uwekezaji na uendashaji wa maduka yake ya kisasa maarufu kama Airtel Money Branch.

Kwa wale ambao watapata fursa hiyo, kampuni ya Airtel itawawezesha kwa kiwapatia vifaa vyotebmuhimu ikiwemo kupiga chapa duka, floti kwenye akaunti ya Airtel Money pamoja na simu za kuendesha duka la Airtel Money kwa mafanikio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza ushirikiano wa uwekezaji huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda alisema kuwa Airtel ina nia ya dhati ya kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kujiajiri kupitia Airtel Money.

Airtel Fursa huwapa vijana fursa ya kuwakilisha ujuzi wao na wangependa kuufanikisha. Mpaka sasa, kuna mamia ya vijana ambao wameweza kufaidikia na kampeini ya Airtel Fursa na mpaka sasa wameweza kujiajiri na hivyo kubadilisha maisha yao. Kupitia Airtel Money branch tuna uhakika maelfu ya vijana wataweza kupata fursa ya kujiajiri na hivyo kubadilisha maisha yao.

Na ikiwa ni muendelezo wa Airtel Tanzania kuendelea kutoa fursa za kujiajiri kwa Watanzania, Airtel pia imeweza kufungua maduka ya huduma za simu mkononi nchini kote. Lengo ni kuendelea kufanya vijana wajiajiri lakini pia ni mpango kabambe wa kupeleka huduma karibu na wateja wake.

Maduka haya ya Airtel Money branch yana muonekano unaofanana na yako katika maeneo maalumu ambayo yatawawezesha maelfu ya wakazi kupata huduma kirahisi na kukidhi mahitaji yao kwa ufanisi zaidi

Maduka hayo yatatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kifedha, huduma za intaneti, kuongeza salio , kusajili namba na pia kuunganisha wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel.

Tunaamini hii ni njia pekee ya kuwafikia wateja wetu na kujua changamoto zao na kuzitatua kwa wakati na vilevile kuwaunganisha na huduma na bidhaa zetu za kipekee na kibunifu zinazosaidia kutatua changamoto zao za kila siku za kijamii na kiuchumi.


Kuanzishwa kwa maduka haya sehemu mbalimbali nchini kunadhihiriwha kwa vitengo dhamira ya Airtel kuendelea kuwekeza nchini na Afrika kwa ujumla.

 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akikata utepe wakati wa kuzindua moja kati ya maduka ya Airtel mkoani shinyanga ambapo jumla ya maduka 8 yatazinduliwa kwa lengo lakutoa ajira na kutoa huduma ya mawasiliano katika mkoa wa Shinyanga. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Airtel Tanzania,  Sunil Colaso akifuatiwa na Meneja wa Kanda ya kati wa Airtel , Bw Stephen Akyoo


Muonekano wa duka jipya la Airtel Money Branch lililopo Wilaya ya Chato mkoani Geita maalum kwa kutoa huduma za mawailiano za Mtandao wa Airtel.

Jumatano, 25 Aprili 2018

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AHUTUBIA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KATIKA UKUMBI WA MSEKWA MKOANI DODOMA


. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wa Wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kwenda kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wa wimbo wa taifa uliokuwa ukipigwa ndani ya ukumbi wa Bunge wa  Msekwa ambapo alihutubia katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) mkoni Dodoma.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki (EALA).Picha namba 8-11. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika mkoni Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuhutubia Bunge la EALA mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa tatu kutoka kulia, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Martin Ngoga wa nne kutoka kulia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuwahutubia mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga mara baada ya kuhutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki linalofanyika mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga mara baada ya kuhutubia Bunge hilo la EALA. PICHA NA IKULU

MAGAZETI LEO JUMATANO 25 APRILI 2018